Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Yakobo 1:15takriban 60 BK

    Basi ile tamaa mbaya ikishachukua mimba, huzaa dhambi, nayo ile dhambi ikikomaa, huzaa mauti.

  2. Yakobo 1:16takriban 60 BK

    Ndugu zangu wapendwa, msidanganyike.

  3. Yakobo 1:17takriban 60 BK

    Kila kitolewacho kilicho chema na kilicho kamili, hutoka juu, na hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.

  4. Yakobo 1:18takriban 60 BK

    Kwa mapenzi yake mwenyewe alituzaa kwa neno la kweli, kusudi tuwe kama mazao ya kwanza katika viumbe vyake vyote.

  5. Yakobo 1:19takriban 60 BK

    Ndugu zangu wapendwa, fahamuni jambo hili: Kila mtu awe mwepesi wa kusikiliza, lakini asiwe mwepesi wa kusema wala wa kukasirika.

  6. Yakobo 1:20takriban 60 BK

    Kwa maana hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu.

  7. Yakobo 1:21takriban 60 BK

    Kwa hiyo, ondoleeni mbali uchafu wote na uovu ambao umezidi kuwa mwingi, mkalipokee kwa unyenyekevu lile Neno lililopandwa ndani yenu ambalo laweza kuokoa nafsi zenu.

  8. Yakobo 1:22takriban 60 BK

    Basi kuweni watendaji wa Neno wala msiwe wasikiaji tu, huku mkijidanganya nafsi zenu.

  9. Yakobo 1:23takriban 60 BK

    Kwa maana kama mtu ni msikiaji tu wa Neno wala hatendi kile linachosema, yeye ni kama mtu ajitazamaye uso wake kwenye kioo

  10. Yakobo 1:24takriban 60 BK

    na baada ya kujiona alivyo, huenda zake na mara husahau jinsi alivyo.

  11. Yakobo 1:25takriban 60 BK

    Lakini yeye anayeangalia kwa bidii katika sheria kamilifu, ile iletayo uhuru, naye akaendelea kufanya hivyo bila kusahau alichosikia, bali akalitenda, atabarikiwa katika kile anachofanya.

  12. Yakobo 1:26takriban 60 BK

    Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hujidanganya moyoni mwake, wala dini yake mtu huyo haifai kitu.

  13. Yakobo 1:27takriban 60 BK

    Dini iliyo safi, isiyo na uchafu, inayokubalika mbele za Mungu Baba yetu, ndiyo hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika dhiki zao na kujilinda usitiwe madoa na dunia.

  14. Yakobo 2:1takriban 60 BK

    Ndugu zangu, kama waaminio katika imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe na upendeleo kwa watu.

  15. Yakobo 2:2takriban 60 BK

    Kwa maana kama akija mtu katika kusanyiko lenu akiwa amevaa pete ya dhahabu na mavazi mazuri, pia akaingia mtu maskini mwenye mavazi yaliyochakaa,

  16. Yakobo 2:3takriban 60 BK

    nanyi mkampa heshima yule aliyevaa mavazi mazuri na kumwambia, “Keti hapa mahali pazuri,” lakini yule maskini mkamwambia, “Wewe simama pale,” au “Keti hapa sakafuni karibu na miguu yangu,”

  17. Yakobo 2:4takriban 60 BK

    je, hamjawabagua na kuwa mahakimu mioyoni mwenu mkihukumu kwa mawazo yenu maovu?

  18. Yakobo 2:5takriban 60 BK

    Ndugu zangu, sikilizeni: Je, Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi Ufalme aliowaahidi wale wampendao?

  19. Yakobo 2:6takriban 60 BK

    Lakini ninyi mmemdharau yule aliye maskini. Je, hao matajiri si ndio wanaowadhulumu na kuwaburuta mahakamani?

  20. Yakobo 2:7takriban 60 BK

    Je, si wao wanaolikufuru Jina lile lililo bora sana mliloitiwa?

  21. Yakobo 2:8takriban 60 BK

    Kama kweli mnaitimiza ile sheria ya kifalme inayopatikana katika Maandiko isemayo, “Mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako,” mnafanya vyema.

  22. Yakobo 2:9takriban 60 BK

    Lakini kama mnakuwa na upendeleo kwa watu, mnatenda dhambi, na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji.

  23. Yakobo 2:10takriban 60 BK

    Kwa maana mtu yeyote anayeishika sheria yote lakini akajikwaa katika kipengele kimoja tu, ana hatia ya kuivunja sheria yote.

  24. Yakobo 2:11takriban 60 BK

    Kwa sababu yeye aliyesema, “Usizini,” alisema pia, “Usiue.” Basi kama huzini lakini unaua, umekuwa mvunjaji wa sheria.

  25. Yakobo 2:12takriban 60 BK

    Hivyo semeni na kutenda kama watu watakaohukumiwa kwa sheria ile iletayo uhuru.