Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Sin

210 mistari · 120 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Huitumia miaka yao katika mafanikio nao hushuka kaburini kwa amani.

  2. Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’ Hatuna haja ya kufahamu njia zako.

  3. Mwenyezi ni nani hata tumtumikie? Tutapata faida gani kumwomba?

  4. Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?

  5. kama nimeifunika dhambi yangu kama wanadamu wengine wafanyavyo, kwa kuficha hatia yangu moyoni mwangu,

  6. Ndipo huja mbele za watu na kusema, ‘Nilitenda dhambi na kupotosha kilichokuwa haki, lakini sikuadhibiwa kama nilivyostahili.

  7. Nifundishe nisichoweza kuona; kama nimekukosea, sitafanya hivyo tena.’

  8. Kwa hiyo najidharau mwenyewe, na kutubu katika mavumbi na majivu.”

  9. Katika hasira yako, usitende dhambi. Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya mkiichunguza mioyo yenu.

  10. Hujivunia tamaa za moyo wake; humbariki mlafi na kumtukana Bwana.

  11. Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau, huficha uso wake na haoni kabisa.”

  12. Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri.

  13. Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi, nazo zisinitawale. Ndipo nitakapokuwa sina lawama, wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa.

  14. Aache uovu, atende mema, aitafute amani na kuifuatilia.

  15. Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu.

  16. Naungama uovu wangu, ninataabishwa na dhambi yangu.

  17. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi. Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; nitaweka lijamu kinywani mwangu wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.”

  18. Mambo haya unayafanya, nami nimekaa kimya, ukafikiri Mimi nami ni kama wewe. Lakini nitakukemea na kuweka mashtaka mbele yako.

  19. Unioshe na uovu wangu wote na unitakase dhambi yangu.

  20. Hakika mimi nilizaliwa mwenye dhambi, mwenye dhambi tangu nilipotungwa mimba kwa mama yangu.

  21. Kila mmoja humtia moyo mwenzake katika mipango mibaya; huzungumza juu ya kuficha mitego yao, nao husema, “Ni nani ataiona?”

  22. Kama ningekuwa nimeyaficha maovu moyoni mwangu, Bwana asingekuwa amenisikiliza;

  23. Ee Bwana, kumbuka jinsi mtesi alivyokudhihaki, jinsi watu wapumbavu walivyolitukana jina lako.

  24. Lakini waliendelea kutenda dhambi dhidi yake, wakiasi jangwani dhidi ya Aliye Juu Sana.

  25. Umeyaweka maovu yetu mbele yako, dhambi zetu za siri katika nuru ya uwepo wako.