Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms

896 mistari · 16 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Heri mtu ambaye podo lake limejazwa nao. Hawataaibishwa wanaposhindana na adui zao langoni.

  2. Wimbo wa kwenda juu. Heri ni wale wote wamchao Bwana, waendao katika njia zake.

  3. Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako.

  4. Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako.

  5. Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Bwana.

  6. Bwana na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu,

  7. nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako. Amani iwe juu ya Israeli.

  8. Wimbo wa kwenda juu. Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa:

  9. wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda.

  10. Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu.

  11. Lakini Bwana ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu.

  12. Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu.

  13. Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua;

  14. kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake.

  15. Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya Bwana iwe juu yako; tunakubariki katika jina la Bwana.”

  16. Wimbo wa kwenda juu. Kutoka vilindini ninakulilia, Ee Bwana.

  17. Ee Bwana, sikia sauti yangu. Masikio yako na yawe masikivu kwa kilio changu unihurumie.

  18. Kama wewe, Ee Bwana, ungeweka kumbukumbu ya dhambi, Ee Bwana, ni nani angeliweza kusimama?

  19. Lakini kwako kuna msamaha, kwa hiyo wewe unaogopwa.

  20. Namngojea Bwana, nafsi yangu inangojea, katika neno lake naweka tumaini langu.

  21. Nafsi yangu inamngojea Bwana kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi, naam, kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi.

  22. Ee Israeli, mtumaini Bwana, maana kwa Bwana kuna upendo usiokoma, na kwake kuna ukombozi kamili.

  23. Yeye mwenyewe ataikomboa Israeli kutoka dhambi zao zote.

  24. Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Moyo wangu hauna kiburi, Ee Bwana, macho yangu hayajivuni; sijishughulishi na mambo makuu kunizidi wala mambo ya ajabu mno kwangu.

  25. Lakini nimetuliza na kunyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa kunyonya na mama yake, kama mtoto aliyeachishwa kunyonya ndivyo ilivyo nafsi iliyoko ndani yangu.