Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms

896 mistari · 16 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao, na kuchochea vita siku zote.

  2. Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka, sumu ya nyoka iko midomoni mwao.

  3. Ee Bwana, niepushe na mikono ya waovu; nilinde na watu wenye jeuri wanaopanga kunikwaza miguu yangu.

  4. Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa, wametandaza kamba za wavu wao, wametega mitego kwenye njia yangu.

  5. Ee Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.” Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia.

  6. Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu, unikingaye kichwa changu siku ya vita:

  7. Ee Bwana, usiwape waovu matakwa yao, usiache mipango yao ikafanikiwa, wasije wakajisifu.

  8. Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe na shida zinazosababishwa na midomo yao.

  9. Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie! Na watupwe motoni, katika mashimo ya matope, wasiinuke tena kamwe.

  10. Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi; maafa na yawawinde watu wenye jeuri.

  11. Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki, na kuitegemeza njia ya mhitaji.

  12. Hakika wenye haki watalisifu jina lako, na waadilifu wataishi mbele zako.

  13. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, ninakuita wewe, uje kwangu hima. Sikia sauti yangu ninapokuita.

  14. Maombi yangu na yafike mbele zako kama uvumba; kuinua mikono yangu juu na kuwe kama dhabihu ya jioni.

  15. Ee Bwana, weka mlinzi kinywani mwangu, weka ulinzi mlangoni mwa midomo yangu.

  16. Usiuache moyo wangu uvutwe katika jambo baya, nisije nikashiriki katika matendo maovu pamoja na watu watendao mabaya, wala nisije nikala vyakula vyao vya anasa.

  17. Mtu mwenye haki na anipige: ni jambo la huruma; na anikemee: ni mafuta kichwani mwangu. Kichwa changu hakitalikataa. Hata hivyo, maombi yangu daima ni kinyume cha watenda mabaya,

  18. watawala wao watatupwa chini kutoka kwenye majabali, waovu watajifunza kwamba maneno yangu yalikuwa kweli.

  19. Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi, ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.”

  20. Lakini nimekaza macho yangu kwako, Ee Bwana Mwenyezi, ndani yako nimekimbilia, usiniache nife.

  21. Niepushe na mitego waliyonitegea, kutokana na mitego iliyotegwa na watenda mabaya.

  22. Waovu na waanguke kwenye nyavu zao wenyewe, wakati mimi ninapita salama.

  23. Utenzi wa Daudi. Alipokuwa pangoni. Maombi. Namlilia Bwana kwa sauti, nainua sauti yangu kwa Bwana anihurumie.

  24. Namimina malalamiko yangu mbele zake, mbele zake naeleza shida zangu.

  25. Wakati roho yangu inapozimia ndani yangu, wewe ndiwe unajua njia zangu. Katika njia ninayopita watu wameniwekea mtego.