Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Psalms

896 mistari · 16 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. kwa Yule awapaye wafalme ushindi, ambaye humwokoa Daudi, mtumishi wake kutokana na upanga hatari.

  2. Nikomboe na uniokoe kutoka mikononi mwa wageni ambao vinywa vyao vimejaa uongo, na mikono yao ya kuume ni midanganyifu.

  3. Kisha wana wetu wakati wa ujana wao watakuwa kama mimea iliyotunzwa vizuri, binti zetu watakuwa kama nguzo zilizoviringwa kurembesha jumba la kifalme.

  4. Ghala zetu zitajazwa aina zote za mahitaji. Kondoo zetu watazaa kwa maelfu, kwa makumi ya maelfu katika mashamba yetu;

  5. maksai wetu watakokota mizigo mizito. Hakutakuwa na kubomoka kuta, hakuna kuchukuliwa mateka, wala kilio cha taabu katika barabara zetu.

  6. Heri watu ambao hili ni kweli; heri wale ambao Bwana ni Mungu wao.

  7. Msifuni Bwana. Msifuni Bwana kutoka mbinguni, msifuni juu vileleni.

  8. Msifuni, enyi malaika wake wote, msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni.

  9. Msifuni yeye, enyi jua na mwezi, msifuni yeye, enyi nyota zote zingʼaazo.

  10. Msifuni yeye, enyi mbingu zilizo juu sana, na ninyi maji juu ya anga.

  11. Vilisifu jina la Bwana kwa maana aliamuru navyo vikaumbwa.

  12. Aliviweka mahali pake milele na milele, alitoa amri ambayo haibadiliki milele.

  13. Mtukuzeni Bwana kutoka duniani, ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari,

  14. umeme wa radi na mvua ya mawe, theluji na mawingu, pepo za dhoruba zinazofanya amri zake,

  15. ninyi milima na vilima vyote, miti ya matunda na mierezi yote,

  16. wanyama wa mwituni na mifugo yote, viumbe vidogo na ndege warukao,

  17. wafalme wa dunia na mataifa yote, ninyi wakuu na watawala wote wa dunia,

  18. wanaume vijana na wanawali, wazee na watoto.

  19. Wote na walisifu jina la Bwana, kwa maana jina lake pekee limetukuka, utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu.

  20. Amewainulia watu wake pembe, sifa ya watakatifu wake wote, ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake. Msifuni Bwana.

  21. Msifuni Bwana. Msifuni Mungu katika patakatifu pake, msifuni katika mbingu zake kuu.

  22. Msifuni kwa matendo yake makuu, msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

  23. Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta, msifuni kwa kinubi na zeze,

  24. msifuni kwa matari na kucheza, msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,

  25. msifuni kwa matoazi yaliayo, msifuni kwa matoazi yavumayo sana.