Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Afflictions

106 mistari · 21 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki; hunipiga shavuni mwangu kwa dharau, na kuungana pamoja dhidi yangu.

  2. Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya, na kunitupa katika makucha ya waovu.

  3. Mambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja; amenikamata shingo na kuniponda. Amenifanya mimi kuwa shabaha yake;

  4. wapiga upinde wake wananizunguka. Bila huruma, huchoma figo zangu, na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi.

  5. Huniponda tena na tena; hunishambulia kama shujaa wa vita.

  6. “Nimejishonea nguo ya gunia juu ya mwili wangu nami nimekizika kipaji cha uso wangu kwenye vumbi.

  7. Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia, macho yangu yamepigwa na giza kuu.

  8. Nguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake, zitalala naye mavumbini.

  9. Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote. Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha.

  10. Kilindi huita kilindi, katika ngurumo za maporomoko ya maji yako; mawimbi yako yote pamoja na viwimbi vimepita juu yangu.

  11. Umetuingiza kwenye nyavu na umetubebesha mizigo mizito migongoni mwetu.

  12. Uliwaruhusu watu watukalie vichwani, tulipita kwenye moto na kwenye maji, lakini ulituleta kwenye nchi iliyojaa utajiri tele.

  13. Hata hivyo alikuwa na huruma, alisamehe maovu yao na hakuwaangamiza. Mara kwa mara alizuia hasira yake, wala hakuchochea ghadhabu yake yote.

  14. Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, upepo upitao ambao haurudi.

  15. Umewalisha kwa mkate wa machozi, umewafanya wanywe machozi bakuli tele.

  16. “Kama wanae wataacha amri yangu na wasifuate sheria zangu,

  17. kama wakihalifu maagizo yangu na kutoshika amri zangu,

  18. nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo, uovu wao kwa kuwapiga,

  19. Yeye hatalaumu siku zote, wala haweki hasira yake milele,

  20. yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.

  21. Mara nyingi aliwaokoa lakini walikuwa wamezama kwenye uasi, nao wakajiharibu katika dhambi zao.

  22. Lakini akaangalia mateso yao wakati aliposikia kilio chao;

  23. kwa ajili yao akakumbuka agano lake, na kutokana na upendo wake mkuu akapooza hasira yake.

  24. Akawafanya wahurumiwe na wote waliowashikilia mateka.

  25. Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki, katika uaminifu wako umeniadhibu.