- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa 1446–1406 BC
The Wilderness Years
Forty years of wandering in the desert test Israel's faith and prepare a new generation to enter the promised land.
Mistari ya kipindi hiki
- Hesabu 13:5takriban 1490 KK
kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;
- Hesabu 13:6takriban 1490 KK
kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;
- Hesabu 13:7takriban 1490 KK
kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yosefu;
- Hesabu 13:8takriban 1490 KK
kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;
- Hesabu 13:9takriban 1490 KK
kutoka kabila la Benyamini, Palti mwana wa Rafu;
- Hesabu 13:10takriban 1490 KK
kutoka kabila la Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi,
- Hesabu 13:11takriban 1490 KK
kutoka kabila la Manase (kabila la Yosefu), Gadi mwana wa Susi;
- Hesabu 13:12takriban 1490 KK
kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemali;
- Hesabu 13:13takriban 1490 KK
kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli;
- Hesabu 13:14takriban 1490 KK
kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Wofsi;
- Hesabu 13:15takriban 1490 KK
kutoka kabila la Gadi, Geueli mwana wa Maki.
- Hesabu 13:16takriban 1490 KK
Haya ndiyo majina ya watu ambao Mose aliwatuma kuipeleleza nchi. (Mose akampa Hoshea mwana wa Nuni jina Yoshua.)
- Hesabu 13:17takriban 1490 KK
Mose alipowatuma wakaipeleleze Kanaani, alisema, “Pandeni kupitia Negebu, mwende mpaka nchi ya vilima.
- Hesabu 13:18takriban 1490 KK
Mwone nchi ni ya namna gani, na kama watu waishio humo wana nguvu au ni wadhaifu, iwapo ni wachache au wengi.
- Hesabu 13:19takriban 1490 KK
Wanaishi katika nchi ya namna gani? Je, ni nzuri au mbaya? Wanaishi katika miji ya namna gani? Je, haina kuta au ngome?
- Hesabu 13:20takriban 1490 KK
Ardhi iko aje? Ina rutuba au la? Je, kuna miti ndani yake au la? Jitahidini kadiri mwezavyo kuleta baadhi ya matunda ya nchi.” (Ulikuwa msimu wa kuiva zabibu za kwanza.)
- Hesabu 13:21takriban 1490 KK
Hivyo wakapanda na kuipeleleza nchi kutoka Jangwa la Sini hadi Rehobu, kuelekea Lebo-Hamathi.
- Hesabu 13:22takriban 1490 KK
Wakapanda kupitia Negebu hadi wakafika Hebroni, mahali ambapo Ahimani, Sheshai na Talmai, wazao wa Anaki, waliishi. (Hebroni ulikuwa umejengwa miaka saba kabla ya mji wa Soani ulioko Misri.)
- Hesabu 13:23takriban 1490 KK
Walipofika katika Bonde la Eshkoli, walivunja tawi lililokuwa na kishada kimoja cha zabibu. Wawili wao wakalichukua lile tawi kwenye mti, pamoja na komamanga na tini.
- Hesabu 13:24takriban 1490 KK
Eneo lile likaitwa Bonde la Eshkoli kwa sababu ya kile kishada cha zabibu ambacho Waisraeli walikikata huko.
- Hesabu 13:25takriban 1490 KK
Mwishoni mwa siku arobaini wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.
- Hesabu 13:26takriban 1490 KK
Wakarudi kwa Mose, Aroni na jumuiya yote ya Waisraeli huko Kadeshi kwenye Jangwa la Parani. Hapo ndipo walipotoa habari kwao na kwa kusanyiko lote na kuwaonyesha matunda ya hiyo nchi.
- Hesabu 13:27takriban 1490 KK
Wakampa Mose taarifa hii: “Tuliingia katika nchi uliyotutuma, nayo inatiririka maziwa na asali! Hili hapa tunda lake.
- Hesabu 13:28takriban 1490 KK
Lakini watu wanaoishi huko ni wenye nguvu, na miji yao ina ngome na ni mikubwa sana. Huko tuliona hata wazao wa Anaki.
- Hesabu 13:29takriban 1490 KK
Waamaleki wanaishi Negebu; Wahiti, Wayebusi na Waamori wanaishi katika nchi ya vilima; nao Wakanaani wanaishi karibu na bahari na kando ya Yordani.”