Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Tito 3:8takriban 65 BK

    Hili ni neno la kuaminiwa. Nami nataka uyasisitize mambo haya, ili wale ambao wamemwamini Mungu wapate kuwa waangalifu kujitoa kwa ajili ya kutenda mema wakati wote. Mambo haya ni mazuri tena ya manufaa kwa kila mtu.

  2. Tito 3:9takriban 65 BK

    Lakini jiepushe na maswali ya kipuzi, mambo ya koo, mabishano na ugomvi kuhusu sheria, kwa sababu hayana faida, tena ni ubatili.

  3. Tito 3:10takriban 65 BK

    Mtu anayesababisha mafarakano, mwonye mara ya kwanza, kisha mwonye mara ya pili. Baada ya hapo, usihusike naye tena.

  4. Tito 3:11takriban 65 BK

    Kwa kuwa unajua kwamba mtu kama huyo amepotoka na tena ni mwenye dhambi. Yeye amejihukumu mwenyewe.

  5. Tito 3:12takriban 65 BK

    Mara nitakapomtuma Artema au Tikiko kwako, jitahidi kuja unione huko Nikopoli, kwa sababu nimeamua kukaa huko wakati wa majira ya baridi.

  6. Tito 3:13takriban 65 BK

    Fanya kila uwezalo uwasafirishe Zena yule mwanasheria na Apolo na uhakikishe kwamba wana kila kitu wanachohitaji katika safari yao.

  7. Tito 3:14takriban 65 BK

    Watu wetu hawana budi kujifunza kutenda mema, ili waweze kuyakimu mahitaji ya kila siku, wasije wakaishi maisha yasiyokuwa na matunda.

  8. Tito 3:15takriban 65 BK

    Wote walio pamoja nami wanakusalimu. Wasalimu wale wanaotupenda katika imani. Neema iwe nanyi nyote. Amen.

  9. Filemoni 1:1takriban 64 BK

    Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, pamoja na Timotheo ndugu yetu: Kwa Filemoni rafiki yetu mpendwa na mtendakazi mwenzetu,

  10. Filemoni 1:2takriban 64 BK

    kwa dada yetu mpendwa Afia, kwa Arkipo askari mwenzetu na kwa kanisa lile likutanalo nyumbani mwako:

  11. Filemoni 1:3takriban 64 BK

    Neema iwe nanyi na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.

  12. Filemoni 1:4takriban 64 BK

    Siku zote ninamshukuru Mungu ninapokukumbuka katika maombi yangu,

  13. Filemoni 1:5takriban 64 BK

    kwa sababu ninasikia juu ya imani yako katika Bwana Yesu na upendo wako kwa watakatifu wote.

  14. Filemoni 1:6takriban 64 BK

    Naomba utiwe nguvu katika kuishuhudia imani yako, ili upate kuwa na ufahamu mkamilifu juu ya kila kitu chema tulicho nacho ndani ya Kristo.

  15. Filemoni 1:7takriban 64 BK

    Upendo wako umenifurahisha mno na kunitia moyo, kwa sababu wewe ndugu, umeiburudisha mioyo ya watakatifu.

  16. Filemoni 1:8takriban 64 BK

    Hata hivyo, ingawa katika Kristo ningeweza kuwa na ujasiri na kukuagiza yale yakupasayo kutenda,

  17. Filemoni 1:9takriban 64 BK

    lakini ninakuomba kwa upendo, mimi Paulo, mzee na pia sasa nikiwa mfungwa wa Kristo Yesu,

  18. Filemoni 1:10takriban 64 BK

    nakuomba kwa ajili ya mwanangu Onesimo, aliyefanyika mwanangu nilipokuwa kwenye minyororo.

  19. Filemoni 1:11takriban 64 BK

    Mwanzoni alikuwa hakufai, lakini sasa anakufaa sana wewe na mimi pia.

  20. Filemoni 1:12takriban 64 BK

    Namtuma kwako, yeye aliye moyo wangu hasa.

  21. Filemoni 1:13takriban 64 BK

    Ningependa nikae naye ili ashike nafasi yako ya kunisaidia wakati huu nikiwa kifungoni kwa ajili ya Injili.

  22. Filemoni 1:14takriban 64 BK

    Lakini sikutaka kufanya lolote bila idhini yako, ili wema wowote uufanyao usiwe wa lazima, bali wa hiari.

  23. Filemoni 1:15takriban 64 BK

    Huenda sababu ya yeye kutengwa nawe kwa kitambo kidogo ni ili uwe naye daima.

  24. Filemoni 1:16takriban 64 BK

    Si kama mtumwa, bali bora kuliko mtumwa, kama ndugu mpendwa. Yeye ni mpendwa sana kwangu na hata kwako zaidi, yeye kama mwanadamu na kama ndugu katika Bwana.

  25. Filemoni 1:17takriban 64 BK

    Hivyo kama unanihesabu mimi kuwa mshirika wako, mkaribishe kama vile ungenikaribisha mimi mwenyewe.