Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 2 Timotheo 4:11takriban 66 BK

    Ni Luka peke yake aliye hapa pamoja nami. Mtafute Marko uje naye kwa sababu ananifaa sana katika huduma yangu.

  2. 2 Timotheo 4:12takriban 66 BK

    Nimemtuma Tikiko huko Efeso.

  3. 2 Timotheo 4:13takriban 66 BK

    Utakapokuja, niletee lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa na vile vitabu vyangu, hasa vile vya ngozi.

  4. 2 Timotheo 4:14takriban 66 BK

    Aleksanda yule mfua chuma alinitendea ubaya mkubwa. Bwana atamlipa kwa ajili ya yale aliyotenda.

  5. 2 Timotheo 4:15takriban 66 BK

    Wewe pia ujihadhari naye kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu.

  6. 2 Timotheo 4:16takriban 66 BK

    Katika utetezi wangu wa mara ya kwanza, hakuna hata mmoja aliyeniunga mkono, bali kila mmoja aliniacha. Namwomba Mungu wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo.

  7. 2 Timotheo 4:17takriban 66 BK

    Lakini Bwana alisimama upande wangu akanitia nguvu, ili kupitia kwangu lile Neno lihubiriwe kwa ukamilifu, watu wote Mataifa wapate kulisikia. Mimi niliokolewa kutoka kinywa cha simba.

  8. 2 Timotheo 4:18takriban 66 BK

    Bwana ataniokoa katika kila shambulio baya na kunileta salama katika Ufalme wake wa mbinguni. Atukuzwe yeye milele na milele. Amen.

  9. 2 Timotheo 4:19takriban 66 BK

    Wasalimu Prisila na Akila, na wote wa nyumbani kwa Onesiforo.

  10. 2 Timotheo 4:20takriban 66 BK

    Erasto alibaki Korintho. Nami nikamwacha Trofimo huko Mileto akiwa mgonjwa.

  11. 2 Timotheo 4:21takriban 66 BK

    Jitahidi ufike huku kabla ya majira ya baridi. Eubulo anakusalimu, vivyo hivyo Pude, Lino, Klaudia na ndugu wote.

  12. 2 Timotheo 4:22takriban 66 BK

    Bwana awe pamoja na roho yako. Neema iwe pamoja nanyi. Amen.

  13. Tito 1:1takriban 65 BK

    Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu na kuijua kweli iletayo utauwa:

  14. Tito 1:2takriban 65 BK

    imani na ujuzi ulioko katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu, asiyesema uongo, aliahidi hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu,

  15. Tito 1:3takriban 65 BK

    naye kwa wakati wake aliouweka alilidhihirisha neno lake kwa njia ya mahubiri ambayo mimi nimewekewa amana kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu:

  16. Tito 1:4takriban 65 BK

    Kwa Tito, mwanangu hasa katika imani tunayoshiriki sote: Neema iwe kwako na amani itokayo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Mwokozi wetu.

  17. Tito 1:5takriban 65 BK

    Sababu ya mimi kukuacha huko Krete ni ili uweke utaratibu mambo yale yaliyosalia na kuwaweka wazee wa kanisa katika kila mji, kama nilivyokuagiza.

  18. Tito 1:6takriban 65 BK

    Mzee wa kanisa asiwe na lawama, awe mume wa mke mmoja, mtu ambaye watoto wake ni waaminio na wala hawashtakiwi kwa ufisadi.

  19. Tito 1:7takriban 65 BK

    Kwa kuwa mwangalizi, kama wakili wa Mungu, imempasa kuwa mtu asiye na lawama, asiwe mwenye majivuno au mwepesi wa hasira, wala mlevi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyo ya halali.

  20. Tito 1:8takriban 65 BK

    Bali awe mkarimu, anayependa mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu, mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake.

  21. Tito 1:9takriban 65 BK

    Inampasa alishike kwa uthabiti lile neno la imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze kuwaonya wengine kwa mafundisho manyofu na kuwakanusha wale wanaopingana nayo.

  22. Tito 1:10takriban 65 BK

    Kwa maana wako wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo na maana, hasa wale wa kikundi cha tohara.

  23. Tito 1:11takriban 65 BK

    Hao ni lazima wanyamazishwe, kwa sababu wanaharibu watu wa nyumba nzima wakifundisha mambo yasiyowapasa kufundisha. Wanafanya hivyo kwa ajili ya kujipatia mapato ya udanganyifu.

  24. Tito 1:12takriban 65 BK

    Hata mmojawapo wa manabii wao mwenyewe amesema, “Wakrete ni waongo siku zote, wanyama wabaya, walafi, wavivu.”

  25. Tito 1:13takriban 65 BK

    Ushuhuda huu ni kweli. Kwa hiyo, uwakemee kwa ukali wapate kuwa wazima katika imani,