Rukia maudhui

circa 2100–1900 BC

Abraham: The Covenant

God calls Abram from Ur, establishes an everlasting covenant, and promises a son through whom all nations will be blessed.

394 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 24:58takriban 1857 KK

    Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumuuliza, “Je, utakwenda na mtu huyu?” Akasema, “Nitakwenda.”

  2. Mwanzo 24:59takriban 1857 KK

    Hivyo wakamwaga ndugu yao Rebeka aondoke, pamoja na mjakazi wake, mtumishi wa Abrahamu na watu wake.

  3. Mwanzo 24:60takriban 1857 KK

    Wakambariki Rebeka, wakamwambia, “Ndugu yetu, uwe wewe kumi elfu, mara elfu nyingi, nao wazao wako wamiliki malango ya adui zao.”

  4. Mwanzo 24:61takriban 1857 KK

    Rebeka na vijakazi wake wakajiandaa, wakapanda ngamia zao wakafuatana na yule mtu. Hivyo yule mtumishi akamchukua Rebeka akaondoka.

  5. Mwanzo 24:62takriban 1857 KK

    Basi Isaki alikuwa ametoka Beer-Lahai-Roi, kwa kuwa alikuwa anaishi nchi ya Negebu.

  6. Mwanzo 24:63takriban 1857 KK

    Isaki akatoka kwenda shambani kutafakari wakati wa jioni, alipoinua macho yake, akaona ngamia wanakuja.

  7. Mwanzo 24:64takriban 1857 KK

    Rebeka pia akainua macho akamwona Isaki. Akashuka kutoka kwenye ngamia wake

  8. Mwanzo 24:65takriban 1857 KK

    na akamuuliza yule mtumishi, “Ni nani mtu yule aliye kule shambani anayekuja kutulaki?” Yule mtumishi akajibu, “Huyu ndiye bwana wangu.” Hivyo Rebeka akachukua shela yake akajifunika.

  9. Mwanzo 24:66takriban 1857 KK

    Kisha yule mtumishi akamweleza Isaki mambo yote aliyoyatenda.

  10. Mwanzo 24:67takriban 1857 KK

    Ndipo Isaki akamwingiza Rebeka katika hema la Sara mama yake, Isaki akamchukua Rebeka, hivyo akawa mke wake. Isaki akampenda, akafarijika baada ya kifo cha mama yake.

  11. Mwanzo 25:1takriban 1853 KK

    Abrahamu alioa mke mwingine, ambaye jina lake aliitwa Ketura.

  12. Mwanzo 25:2takriban 1852 KK

    Huyu alimzalia Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua.

  13. Mwanzo 25:3takriban 1824 KK

    Yokshani alikuwa baba wa Sheba na Dedani, wazao wa Dedani walikuwa Waashuri, Waletushi na Waleumi.

  14. Mwanzo 25:4takriban 1804 KK

    Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. Hawa wote walikuwa uzao wa Ketura.

  15. Mwanzo 25:5takriban 1829 KK

    Abrahamu akamwachia Isaki kila kitu alichokuwa nacho.

  16. Mwanzo 25:6takriban 1829 KK

    Lakini Abrahamu alipokuwa bado hai, akawapa watoto wa masuria wake zawadi, kisha akawaondoa waende kuishi pande za mashariki mbali na mwanawe Isaki.

  17. Mwanzo 25:7takriban 1821 KK

    Kwa jumla, Abrahamu aliishi miaka 175.

  18. Mwanzo 25:8takriban 1821 KK

    Ndipo Abrahamu akapumua pumzi ya mwisho na akafa akiwa mwenye umri mzuri, mzee aliyeshiba siku, naye akakusanywa pamoja na watu wake.

  19. Mwanzo 25:9takriban 1821 KK

    Watoto wake Isaki na Ishmaeli wakamzika katika pango la Makpela karibu na Mamre, katika shamba lililokuwa la Efroni mwana wa Sohari Mhiti,

  20. Mwanzo 25:10takriban 1821 KK

    Shamba ambalo Abrahamu alilinunua kwa Wahiti. Hapo ndipo Abrahamu alipozikwa pamoja na mkewe Sara.

  21. Mwanzo 25:11takriban 1821 KK

    Baada ya kifo cha Abrahamu, Mungu akambariki mwanawe Isaki, ambaye baadaye aliishi karibu na Beer-Lahai-Roi.

  22. Mwanzo 25:12takriban 1821 KK

    Hivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli mtoto wa Abrahamu, ambaye mjakazi wake Sara, Hagari Mmisri, alimzalia Abrahamu.

  23. Mwanzo 25:13takriban 1821 KK

    Haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, yaliyoorodheshwa kulingana na jinsi walivyozaliwa: Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli ni Nebayothi, akafuatia Kedari, Adbeeli, Mibsamu,

  24. Mwanzo 25:14takriban 1821 KK

    Mishma, Duma, Masa,

  25. Mwanzo 25:15takriban 1821 KK

    Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema.