Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Wine

175 mistari · 83 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Wanakula mkate wa uovu, na kunywa mvinyo wa jeuri.

  2. Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake; pia ameandaa meza yake.

  3. Njooni, mle chakula changu na mnywe divai niliyoichanganya.

  4. Mvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi; yeyote apotoshwaye navyo hana hekima.

  5. Mtu apendaye anasa atakuwa maskini, yeyote apendaye mvinyo na mafuta kamwe hatakuwa tajiri.

  6. Ni nani mwenye ole? Ni nani mwenye huzuni? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye malalamiko? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani mwenye macho mekundu?

  7. Ni hao wakaao sana kwenye mvinyo, hao waendao kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa.

  8. Usiukodolee macho mvinyo wakati ukiwa mwekundu, wakati unapometameta kwenye bilauri, wakati ushukapo taratibu!

  9. Mwishowe huuma kama nyoka na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu.

  10. “Ee Lemueli, haifai wafalme, haifai wafalme kunywa mvinyo, haifai watawala kutamani sana kileo,

  11. wasije wakanywa na kusahau vile sheria inavyoamuru na kuwanyima haki zao wote walioonewa.

  12. Wape kileo wale wanaoangamia, mvinyo wale walio na uchungu,

  13. Wanywe na kusahau umaskini wao na wasikumbuke taabu yao tena.

  14. Nikajaribu kujifurahisha kwa mvinyo na kukumbatia upumbavu, huku bado akili yangu inaniongoza kwa hekima. Nilitaka kuona ni lipi bora watu wafanye kwa siku chache wanazoishi chini ya mbingu.

  15. Hata hivyo nilipokuja kuangalia yote ambayo mikono yangu ilikuwa imefanya na yale niliyotaabika kukamilisha, kila kitu kilikuwa ni ubatili, ni kukimbiza upepo; hapakuwa na faida yoyote chini ya jua.

  16. Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, nao mvinyo hufurahisha maisha, lakini fedha ni jawabu la mambo yote.

  17. Unibusu kwa busu la kinywa chako, kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai.

  18. Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Marafiki Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Mpendwa Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!

  19. Nitie nguvu kwa zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, kwa maana ninazimia kwa mapenzi.

  20. Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu; nimekusanya manemane yangu pamoja na kikolezo changu. Nimekula sega langu la asali na asali yangu; nimekunywa divai yangu na maziwa yangu. Marafiki Kuleni, enyi marafiki, mnywe; kunyweni ya kutosha, ee wapenzi.

  21. Ningelikuongoza na kukuleta katika nyumba ya mama yangu, yeye ambaye amenifundisha. Ningelikupa divai iliyokolezwa unywe, asali ya maua ya mikomamanga yangu.

  22. Fedha yenu imekuwa takataka, divai yenu nzuri imechanganywa na maji.

  23. Ole wao wale waamkao asubuhi na mapema wakikimbilia kunywa vileo, wale wakawiao sana mpaka usiku, mpaka wamewaka kwa mvinyo.

  24. Wana vinubi na zeze kwenye karamu zao, matari, filimbi na mvinyo, lakini hawayajali matendo ya Bwana, wala hawana heshima kwa ajili ya kazi ya mikono yake.

  25. Ole wao walio mashujaa kwa kunywa mvinyo, nao walio hodari katika kuchanganya vileo,