Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Wine: Moab

5 mistari · 83 vipengele

Mistari kuhusu Moab

  1. Mashamba ya Heshboni yananyauka, pia na mizabibu ya Sibma. Watawala wa mataifa wamekanyaga mizabibu iliyo mizuri sana, ambayo ilipata kufika Yazeri na kuenea kuelekea jangwani. Machipukizi yake yalienea yakafika hadi baharini.

  2. Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo, kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Ee Heshboni, ee Eleale, ninakulowesha kwa machozi! Kelele za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa.

  3. Furaha na shangwe zimeondolewa kutoka mashamba ya matunda; hakuna yeyote aimbaye wala apazaye sauti katika mashamba ya mizabibu; hakuna yeyote akanyagaye zabibu shinikizoni, kwa kuwa nimekomesha makelele.

  4. Ninalia machozi kwa ajili yenu, kama Yazeri aliavyo, enyi mizabibu ya Sibma. Matawi yako yameenea hadi baharini; yamefika hadi bahari ya Yazeri. Mharabu ameyaangukia matunda yako yaliyoiva na mizabibu yako iliyoiva.

  5. Shangwe na furaha vimetoweka kutoka bustani na mashamba ya Moabu. Nimekomesha kutiririka kwa divai kutoka mashinikizo; hakuna hata mmoja ayakanyagaye kwa kelele za shangwe. Ingawa kuna kelele, sio kelele za shangwe.