Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Prayer

720 mistari · 120 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana, unihurumie na unijibu.

  2. Moyo wangu unasema kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Uso wako, Bwana “Nitautafuta.”

  3. Usinifiche uso wako, usimkatae mtumishi wako kwa hasira; wewe umekuwa msaada wangu. Usinikatae wala usiniache, Ee Mungu Mwokozi wangu.

  4. Zaburi ya Daudi. Ninakuita wewe, Ee Bwana, Mwamba wangu; usiwe kwangu kama kiziwi. Kwa sababu ukinyamaza nitafanana na walioshuka shimoni.

  5. Sikia kilio changu unihurumie ninapokuita kwa ajili ya msaada, niinuapo mikono yangu kuelekea Patakatifu pa Patakatifu pako.

  6. Walipe sawasawa na matendo yao, sawasawa na matendo yao maovu; walipe sawasawa na kazi za mikono yao, uwalipe wanavyostahili.

  7. Bwana asifiwe, kwa maana amesikia kilio changu nikimwomba anihurumie.

  8. Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya.

  9. Ee Bwana, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.

  10. Kwa kuwa wewe ni mwamba wangu na ngome yangu, uniongoze na kunilinda kwa ajili ya jina lako.

  11. Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi, naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali; nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso, na mifupa yangu inachakaa.

  12. Usiniache niaibike, Ee Bwana, kwa maana nimekulilia wewe, bali waovu waaibishwe na kunyamazishwa Kuzimu.

  13. Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe, kwa maana kwa kiburi na dharau wao husema kwa majivuno dhidi ya wenye haki.

  14. Katika hofu yangu nilisema, “Nimekatiliwa mbali na macho yako!” Hata hivyo ulisikia kilio changu ukanihurumia nilipokuita unisaidie.

  15. Niliponyamaza, mifupa yangu ilichakaa kwa kulia kwa maumivu makali mchana kutwa.

  16. Kisha nilikujulisha dhambi yangu wala sikuficha uovu wangu. Nilisema, “Nitaungama makosa yangu kwa Bwana.” Ndipo uliponisamehe hatia ya dhambi yangu.

  17. Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombe wakati unapopatikana, hakika maji makuu yatakapofurika hayatamfikia yeye.

  18. Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote.

  19. Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.

  20. Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote.

  21. Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.

  22. Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote.

  23. Wafedheheshwe na waaibishwe wale wanaotafuta uhai wangu. Wanaofanya shauri kuniangamiza warudishwe nyuma kwa hofu.

  24. maafa na yawapate ghafula: wavu walionifichia na uwatege wenyewe, na waanguke katika shimo hilo, kwa maangamizo yao.

  25. Ee Bwana, umeona hili, usiwe kimya. Usiwe mbali nami, Ee Bwana.