Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Holy Land

108 mistari · 37 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Mpaka utaelekea kusini kuanzia Shefamu hadi Ribla upande wa mashariki wa Aini, na kuendelea kwenye miteremko mashariki mwa Bahari ya Kinerethi.

  2. Kisha mpaka utashuka kuelekea Mto Yordani na kuishia katika Bahari ya Chumvi. “ ‘Hii itakuwa nchi yenu, ikiwa na mipaka yake kila upande.’ ”

  3. Bwana akamwambia Mose,

  4. “Haya ndiyo majina ya watu ambao watakusaidia kugawanya nchi kama urithi: Eleazari kuhani na Yoshua mwana wa Nuni.

  5. Tena uteue kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia kuigawanya nchi.

  6. Haya ndiyo majina yao: “Kalebu mwana wa Yefune, kutoka kabila la Yuda;

  7. Shemueli mwana wa Amihudi, kutoka kabila la Simeoni;

  8. Elidadi mwana wa Kisloni, kutoka kabila la Benyamini;

  9. Buki mwana wa Yogli, kiongozi kutoka kabila la Dani;

  10. Hanieli mwana wa Efodi, kiongozi kutoka kabila la Manase mwana wa Yosefu;

  11. Kemueli mwana wa Shiftani, kiongozi kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yosefu;

  12. Elisafani mwana wa Parnaki, kiongozi kutoka kabila la Zabuloni;

  13. Paltieli mwana wa Azani, kiongozi kutoka kabila la Isakari;

  14. Ahihudi mwana wa Shelomi, kiongozi kutoka kabila la Asheri;

  15. Pedaheli mwana wa Amihudi, kiongozi kutoka kabila la Naftali.”

  16. Hawa ndio watu ambao Bwana aliamuru wagawanye urithi kwa Waisraeli katika nchi ya Kanaani.

  17. Kwa kuwa Bwana Mungu wenu anawaleta katika nchi nzuri, nchi yenye vijito na mabwawa ya maji, yenye chemchemi zinazotiririka mabondeni na katika vilima;

  18. nchi yenye ngano na shayiri, mizabibu na mitini, mikomamanga, mafuta ya zeituni na asali;

  19. nchi ambayo chakula hakitapungua na hamtakosa chochote; nchi ambayo miamba yake ni chuma na mnaweza kuchimba shaba kutoka kwenye vilima.

  20. Nchi mnayoiingia kuimiliki haifanani na nchi ya Misri mlikotoka ambako mlipanda mbegu yenu na kuinywesha, kama bustani ya mboga.

  21. Lakini nchi mnayovuka Yordani kuimiliki ni nchi ya milima na mabonde inywayo mvua kutoka mbinguni.

  22. Ni nchi ambayo Bwana Mungu wenu anaitunza; macho ya Bwana Mungu wenu yanaitazama daima kutoka mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka.

  23. Kama mkishika kwa makini maagizo haya yote ninayowapa kuyafuata, ya kumpenda Bwana Mungu wenu, kuenenda katika njia zake zote na kushikamana naye kwa uthabiti,

  24. ndipo Bwana atawafukuza mataifa haya yote mbele yako, nawe utawafukuza mataifa yaliyo makubwa na yenye nguvu kukuliko wewe.

  25. Kila mahali mtakapoweka mguu wenu patakuwa penu: Nchi yenu itaenea kutoka jangwa la Lebanoni, na kutoka mto wa Frati hadi bahari ya magharibi