Skip to content

Asher

43 mistari · 19 wanafamilia

Anajulikana pia kama: Aser

Mistari inayomtaja Asher

Chuja kwa kitabu
  1. Ndipo Lea aliposema, “Jinsi gani nilivyo na furaha! Wanawake wataniita furaha.” Kwa hiyo akamwita Asheri.

  2. Wana waliozaliwa na Zilpa mtumishi wa kike wa Lea walikuwa: Gadi na Asheri. Hawa walikuwa wana wa Yakobo, waliozaliwa kwake akiwa Padan-Aramu.

  3. Wana wa Asheri ni: Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera. Wana wa Beria ni: Heberi na Malkieli.

  4. “Chakula cha Asheri kitakuwa kinono, naye atatoa chakula kitamu kimfaacho mfalme.

  5. Dani na Naftali, Gadi na Asheri.

  6. kutoka Asheri, ni Pagieli mwana wa Okrani;

  7. Kutoka wazao wa Asheri: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.

  8. Idadi kutoka kabila la Asheri walikuwa watu 41,500.

  9. Kabila la Asheri watapiga kambi karibu na Dani. Kiongozi wa watu wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okrani.

  10. Siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, kiongozi wa watu wa Asheri, alileta sadaka yake.

  11. Pagieli mwana wa Okrani aliongoza kikosi cha kabila la Asheri,

  12. kutoka kabila la Asheri, Sethuri mwana wa Mikaeli;

  13. Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Imna, ukoo wa Waimna; kutoka kwa Ishvi, ukoo wa Waishvi; kutoka kwa Beria, ukoo wa Waberia;

  14. (Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.)

  15. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa 53,400.

  16. Ahihudi mwana wa Shelomi, kiongozi kutoka kabila la Asheri;

  17. Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali.

  18. Kuhusu Asheri akasema: “Aliyebarikiwa zaidi sana katika wana ni Asheri; yeye na apate upendeleo kwa ndugu zake, yeye na anawe miguu yake kwenye mafuta.

  19. Eneo la Manase lilienea kuanzia Asheri hadi Mikmeta mashariki mwa Shekemu. Mpaka ule ulielekea upande wa kusini kutoka pale kujumuisha watu walioishi En-Tapua.

  20. Nchi ya kusini ilikuwa ya Efraimu, na ile iliyokuwa upande wa kaskazini ilikuwa ya Manase. Eneo la Manase lilifika bahari na ikapakana na Asheri upande wa kaskazini, na Isakari upande wa mashariki.

  21. Katika Isakari na Asheri Manase alikuwa na miji pia: Beth-Shani, Ibleamu na watu wa Dori, Endori, Taanaki na Megido, pamoja na vijiji vyote vinavyohusika na miji hiyo (ya tatu katika orodha ni Nafothi).

  22. Kura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.

  23. Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa ndio urithi wa kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.

  24. Mpaka ukaendelea magharibi kupitia Aznoth-Tabori na kutokea Hukoki. Ukagusa Zabuloni upande wa kusini, Asheri upande wa magharibi, na Yordani upande wa mashariki.

  25. Wazao wa Gershoni walipewa miji kumi na mitatu kutoka koo za makabila ya Isakari, Asheri, Naftali na nusu ya Manase huko Bashani.