Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Tribe Of Asher

29 mistari · 21 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Siku ya kumi na moja Pagieli mwana wa Okrani, kiongozi wa watu wa Asheri, alileta sadaka yake.

  2. Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka;

  3. sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

  4. fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja na mwana-kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja, kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

  5. mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi;

  6. maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani.

  7. Wazao wa Asheri kwa koo zao walikuwa: kutoka kwa Imna, ukoo wa Waimna; kutoka kwa Ishvi, ukoo wa Waishvi; kutoka kwa Beria, ukoo wa Waberia;

  8. kutoka kwa wazao wa Beria: kutoka kwa Heberi, ukoo wa Waheberi; kutoka kwa Malkieli, ukoo wa Wamalkieli.

  9. (Asheri alikuwa na binti aliyeitwa Sera.)

  10. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Asheri; wale waliohesabiwa walikuwa 53,400.

  11. Kura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.

  12. Eneo lao lilijumuisha: Helkathi, Hali, Beteni, Akishafu,

  13. Alameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi.

  14. Tena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto.

  15. Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu.

  16. Mpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika eneo la Akzibu,

  17. Uma, Afeki na Rehobu. Ilikuwepo miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.

  18. Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa ndio urithi wa kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.

  19. Wana wa Asheri walikuwa: Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera.

  20. Wana wa Beria walikuwa: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi.

  21. Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao.

  22. Wana wa Yafleti walikuwa: Pasaki, Bimhali na Ashvathi. Hawa walikuwa wana wa Yafleti.

  23. Wana wa Shemeri walikuwa: Ahi, Roga, Yehuba na Aramu.

  24. Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa: Sofa, Imna, Sheleshi na Amali.

  25. Wana wa Sofa walikuwa: Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra,