Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Tribe Of Asher: Bounds of their inheritance

8 mistari · 21 vipengele

Mistari kuhusu Bounds of their inheritance

  1. Kura ya tano ikaangukia kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.

  2. Eneo lao lilijumuisha: Helkathi, Hali, Beteni, Akishafu,

  3. Alameleki, Amadi na Mishali. Upande wa magharibi mpaka uligusa Karmeli na Shihor-Libnathi.

  4. Tena ukageuka mashariki kuelekea Beth-Dagoni, ukagusa Zabuloni na Bonde la Ifta-Eli, ukaenda upande wa kaskazini hadi Beth-Emeki na Neyeli, ukipitia Kabul upande wa kushoto.

  5. Ukaendelea hadi Abdoni, Rehobu, Hamoni na Kana, na kufika Sidoni Kuu.

  6. Mpaka huo ukageukia nyuma kuelekea Rama na kwenda hadi kwenye mji wenye ngome wa Tiro, ukageuka kuelekea Hosa na kutokeza baharini katika eneo la Akzibu,

  7. Uma, Afeki na Rehobu. Ilikuwepo miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.

  8. Miji hii pamoja na vijiji vyake ilikuwa ndio urithi wa kabila la Asheri, ukoo kwa ukoo.