Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Holy Land: Divided by lot

22 mistari · 37 vipengele

Mistari kuhusu Divided by lot

  1. Bwana akamwambia Mose,

  2. “Haya ndiyo majina ya watu ambao watakusaidia kugawanya nchi kama urithi: Eleazari kuhani na Yoshua mwana wa Nuni.

  3. Tena uteue kiongozi mmoja kutoka kila kabila kusaidia kuigawanya nchi.

  4. Haya ndiyo majina yao: “Kalebu mwana wa Yefune, kutoka kabila la Yuda;

  5. Shemueli mwana wa Amihudi, kutoka kabila la Simeoni;

  6. Elidadi mwana wa Kisloni, kutoka kabila la Benyamini;

  7. Buki mwana wa Yogli, kiongozi kutoka kabila la Dani;

  8. Hanieli mwana wa Efodi, kiongozi kutoka kabila la Manase mwana wa Yosefu;

  9. Kemueli mwana wa Shiftani, kiongozi kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yosefu;

  10. Elisafani mwana wa Parnaki, kiongozi kutoka kabila la Zabuloni;

  11. Paltieli mwana wa Azani, kiongozi kutoka kabila la Isakari;

  12. Ahihudi mwana wa Shelomi, kiongozi kutoka kabila la Asheri;

  13. Pedaheli mwana wa Amihudi, kiongozi kutoka kabila la Naftali.”

  14. Hawa ndio watu ambao Bwana aliamuru wagawanye urithi kwa Waisraeli katika nchi ya Kanaani.

  15. sasa basi, ligawanye eneo hili kwa yale makabila tisa na ile nusu ya kabila la Manase kuwa urithi.”

  16. Ile nusu nyingine ya Manase, Wareubeni na Wagadi, walishapokea urithi Mose aliokuwa amewapa mashariki mwa Yordani, sawasawa na mtumishi wa Bwana alivyowagawia.

  17. Eneo lao lilienea toka Aroeri, iliyoko ukingoni mwa Bonde la Arnoni kuanzia mji ulio katikati ya bonde, likijumlisha nchi ya uwanda wa juu wote wa Medeba mpaka Diboni,

  18. nayo miji yote ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala Heshboni, hadi mpakani mwa Waamoni.

  19. Vilevile ilijumlisha Gileadi, eneo la Wageshuri na Wamaaka, mlima wote wa Hermoni na Bashani yote ikienea hadi Saleka:

  20. yaani ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyekuwa ametawala katika Ashtarothi na Edrei, na ndiye pekee alisalia kwa Warefai. Mose alikuwa amewashinda na kuteka nchi yao.

  21. Lakini Waisraeli hawakuwafukuza watu wa Geshuri na wa Maaka, kwa hiyo wanaendelea kuishi miongoni mwa Waisraeli mpaka leo hii.

  22. Lakini kwa kabila la Lawi, Mose hakupeana urithi, kwa kuwa sadaka za kuteketezwa kwa moto zilizotolewa kwa Bwana, Mungu wa Israeli, ndizo zilizokuwa urithi wao, kama alivyowaahidi.