Rukia maudhui

circa 1010–970 BC

The Reign of David

David unites the tribes, conquers Jerusalem, and establishes Israel's golden age—even through deep personal failure.

1,230 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 2 Samweli 14:17takriban 1027 KK

    “Basi sasa mtumishi wako anasema, ‘Neno la bwana wangu mfalme na linipatie pumziko, kwa maana bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu katika kutambua jema na baya. Bwana Mungu wako na awe pamoja nawe.’ ”

  2. 2 Samweli 14:18takriban 1027 KK

    Basi mfalme akamwambia huyo mwanamke, “Usinifiche jibu kuhusu hilo nitakalokuuliza.” Huyo mwanamke akasema, “Mfalme bwana wangu na aseme.”

  3. 2 Samweli 14:19takriban 1027 KK

    Mfalme akauliza, “Je, mkono wa Yoabu haupo pamoja nawe katika jambo hilo lote?” Huyo mwanamke akajibu, “Hakika kama uishivyo, bwana wangu mfalme, hakuna yeyote anayeweza kugeuka kulia wala kushoto kutokana na chochote anachosema bwana wangu mfalme. Naam, ni mtumishi wako Yoabu ndiye alinifundisha kufanya hivi, naye ndiye aliweka maneno haya yote kinywani mwa mtumishi wako.

  4. 2 Samweli 14:20takriban 1027 KK

    Mtumishi wako Yoabu amefanya hivi ili kubadili hali iliyopo. Bwana wangu ana hekima kama ile ya malaika wa Mungu, hufahamu kila kitu kinachotokea katika nchi.”

  5. 2 Samweli 14:21takriban 1027 KK

    Mfalme akamwambia Yoabu, “Vyema sana, nitalifanya jambo hili. Nenda, ukamlete kijana Absalomu.”

  6. 2 Samweli 14:22takriban 1027 KK

    Yoabu akaanguka kifudifudi mpaka ardhini kumpa mfalme heshima, naye akambariki mfalme. Yoabu akasema, “Leo mtumishi wako anajua kuwa amepata kibali machoni pako, bwana wangu mfalme, kwa sababu mfalme amemjalia mtumishi wake ombi lake.”

  7. 2 Samweli 14:23takriban 1027 KK

    Ndipo Yoabu akaenda hadi Geshuri akamrudisha Absalomu Yerusalemu.

  8. 2 Samweli 14:24takriban 1027 KK

    Lakini mfalme akasema, “Lazima Absalomu aende kwenye nyumba yake mwenyewe; kamwe asiuone uso wangu.” Kwa hiyo Absalomu akaenda kwenye nyumba yake na hakuuona uso wa mfalme.

  9. 2 Samweli 14:25takriban 1027 KK

    Katika Israeli yote hakuna mtu yeyote aliyesifiwa kwa uzuri wa sura kama Absalomu. Kuanzia utosi wa kichwa chake hadi wayo wa mguu wake hapakuwa na kasoro.

  10. 2 Samweli 14:26takriban 1027 KK

    Kila mara aliponyoa nywele za kichwa chake, kwa kuwa alikuwa akinyoa mara kwa mara zilipokuwa zinamwia nzito, alizipima uzito wake ulikuwa shekeli mia mbili kwa kipimo cha kifalme.

  11. 2 Samweli 14:27takriban 1027 KK

    Walizaliwa wana watatu na binti mmoja kwa Absalomu. Jina la binti yake aliitwa Tamari, naye akawa mwanamke mzuri wa sura.

  12. 2 Samweli 14:28takriban 1027 KK

    Absalomu akaishi miaka miwili huko Yerusalemu pasipo kuuona uso wa mfalme.

  13. 2 Samweli 14:29takriban 1027 KK

    Basi Absalomu akamwita Yoabu kwa kusudi la kumtuma kwa mfalme, lakini Yoabu akakataa kuja kwa Absalomu. Ndipo akamwita tena mara ya pili, lakini pia akakataa kuja.

  14. 2 Samweli 14:30takriban 1027 KK

    Ndipo akawaambia watumishi wake, “Tazama, shamba la Yoabu liko jirani na langu, naye ana shayiri humo. Nendeni mkalitie moto.” Kisha watumishi wa Absalomu wakalitia moto shamba hilo.

  15. 2 Samweli 14:31takriban 1027 KK

    Basi Yoabu akaenda nyumbani kwa Absalomu, akamwambia, “Kwa nini watumishi wako wametia moto shamba langu?”

  16. 2 Samweli 14:32takriban 1027 KK

    Absalomu akamwambia Yoabu, “Tazama, nilikutumia ujumbe na kusema, ‘Njoo ili niweze kukutuma kwa mfalme kuuliza, “Kwa nini nimekuja kutoka Geshuri? Ingekuwa bora zaidi kwangu kama ningebaki huko!” ’ Sasa basi, nataka kuuona uso wa mfalme, na ikiwa nina hatia ya jambo lolote, basi na aniue.”

  17. 2 Samweli 14:33takriban 1025 KK

    Basi Yoabu akaenda kwa mfalme na kumwambia jambo hili. Kisha mfalme akamwita Absalomu, naye akaingia ndani akasujudu uso wake mpaka ardhini mbele ya mfalme. Naye mfalme akambusu Absalomu.

  18. 2 Samweli 15:1takriban 1024 KK

    Baada ya muda, Absalomu akajipatia magari ya vita na farasi pamoja na watu hamsini wa kupiga mbio mbele yake.

  19. 2 Samweli 15:2takriban 1024 KK

    Akawa anaamka asubuhi na mapema na kusimama kando ya barabara inayoelekea kwenye lango la mji. Wakati wowote alipokuja mtu yeyote mwenye mashtaka yanayohitaji kuletwa mbele ya mfalme kwa maamuzi, Absalomu naye angemwita na kumuuliza, “Wewe unatoka mji upi?” Naye angejibu, “Mtumishi wako anatoka katika mojawapo ya makabila ya Israeli.”

  20. 2 Samweli 15:3takriban 1024 KK

    Kisha Absalomu angemwambia, “Tazama, malalamiko yako ni ya haki na sawasawa, lakini hakuna mwakilishi wa mfalme wa kukusikiliza.”

  21. 2 Samweli 15:4takriban 1024 KK

    Absalomu aliongeza, “Laiti tu ningeteuliwa kuwa mwamuzi katika nchi. Ndipo kila mmoja mwenye mashtaka au shauri angekuja kwangu nami ningeona kwamba anapata haki.”

  22. 2 Samweli 15:5takriban 1024 KK

    Pia, wakati mtu yeyote alipomkaribia ili kusujudu mbele yake, Absalomu alinyoosha mkono wake na kumshika pia kumbusu.

  23. 2 Samweli 15:6takriban 1024 KK

    Absalomu akaendelea na tabia hii mbele ya Waisraeli wote waliomjia mfalme kumwomba awape haki; kwa hiyo Absalomu akaiba mioyo ya watu wa Israeli.

  24. 2 Samweli 15:7takriban 1021 KK

    Mnamo mwisho wa mwaka wa nne, Absalomu akamwambia mfalme, “Naomba unipe ruhusa niende Hebroni nikatimize nadhiri niliyomwekea Bwana.

  25. 2 Samweli 15:8takriban 1021 KK

    Wakati mtumishi wako alipokuwa huko Geshuri katika nchi ya Aramu, niliweka nadhiri hii, ‘Ikiwa Bwana atanirudisha Yerusalemu, nitamwabudu Bwana huko Hebroni.’ ”