Rukia maudhui

circa 1010–970 BC

The Reign of David

David unites the tribes, conquers Jerusalem, and establishes Israel's golden age—even through deep personal failure.

1,230 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 2 Samweli 15:9takriban 1021 KK

    Mfalme akamwambia, “Enenda kwa amani.” Hivyo akaenda Hebroni.

  2. 2 Samweli 15:10takriban 1021 KK

    Kisha Absalomu akatuma wajumbe kwa siri katika makabila yote ya Israeli, kusema, “Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta basi semeni, ‘Absalomu ni mfalme huko Hebroni.’ ”

  3. 2 Samweli 15:11takriban 1021 KK

    Watu mia mbili kutoka Yerusalemu walikuwa wamefuatana na Absalomu. Walikuwa wamealikwa kama wageni nao walikwenda kwa nia njema, pasipo kujua lolote.

  4. 2 Samweli 15:12takriban 1021 KK

    Wakati Absalomu alipokuwa anatoa dhabihu, pia akatuma aitwe Ahithofeli, Mgiloni, mshauri wa Daudi, aje kutoka Gilo, ambao ndio mji wake wa nyumbani. Kwa hiyo mpango wa hila ukapata nguvu, na idadi ya waliofuatana na Absalomu ikaongezeka.

  5. 2 Samweli 15:13takriban 1021 KK

    Mjumbe akaja na kumwambia Daudi, “Mioyo ya watu wa Israeli inaambatana na Absalomu.”

  6. 2 Samweli 15:14takriban 1021 KK

    Ndipo Daudi akawaambia maafisa wake wote waliokuwa pamoja naye huko Yerusalemu, “Njooni! Ni lazima tukimbie, la sivyo hakuna hata mmoja wetu atakayeokoka kutoka mkononi mwa Absalomu. Ni lazima tuondoke kwa haraka, la sivyo atakuja mbio na kutupata, atatuangamiza na kuupiga mji kwa upanga.”

  7. 2 Samweli 15:15takriban 1021 KK

    Maafisa wa mfalme wakamjibu, “Watumishi wako tu tayari kufanya lolote mfalme bwana wetu analochagua.”

  8. 2 Samweli 15:16takriban 1021 KK

    Mfalme akatoka, pamoja na watu wa nyumbani mwake wakimfuata; lakini akawaacha masuria kumi ili kuangalia jumba la kifalme.

  9. 2 Samweli 15:17takriban 1021 KK

    Hivyo mfalme akaondoka, pamoja na watu wote wakimfuata, wakatua mahali mbali kiasi.

  10. 2 Samweli 15:18takriban 1021 KK

    Watu wake wote wakatembea, wakampita wakiwa wamefuatana na Wakerethi na Wapelethi wote; pia Wagiti wote mia sita waliokuwa wamefuatana naye kutoka Gathi wakapita mbele ya mfalme.

  11. 2 Samweli 15:19takriban 1021 KK

    Mfalme akamwambia Itai, Mgiti, “Kwa nini ufuatane na sisi? Rudi ukakae pamoja na Mfalme Absalomu. Wewe ni mgeni, mkimbizi kutoka nchini mwako.

  12. 2 Samweli 15:20takriban 1021 KK

    Ulikuja jana tu. Nami leo nikufanye utangetange pamoja nasi, wakati sijui niendako? Rudi, nawe ukawachukue watu wa kwenu. Wema na uaminifu na viwe pamoja nawe.”

  13. 2 Samweli 15:21takriban 1021 KK

    Lakini Itai akamjibu mfalme, “Hakika kama Bwana aishivyo na kama mfalme bwana wangu aishivyo, popote mfalme bwana wangu atakapokuwa, ikiwa ni kuishi au kufa, hapo ndipo mtumishi wako atakapokuwa.”

  14. 2 Samweli 15:22takriban 1021 KK

    Daudi akamwambia Itai, “Songa mbele, endelea.” Kwa hiyo Itai, Mgiti, akaendelea pamoja na watu wake wote, pia jamaa zote waliokuwa pamoja naye.

  15. 2 Samweli 15:23takriban 1021 KK

    Watu wote wa nje ya mji wakalia kwa sauti wakati watu wote walipokuwa wakipita. Mfalme naye akavuka Bonde la Kidroni, nao watu wote wakaelekea jangwani.

  16. 2 Samweli 15:24takriban 1021 KK

    Sadoki pia alikuwako, kadhalika Walawi wote waliokuwa pamoja naye walikuwa wamechukua Sanduku la Agano la Mungu. Wakaweka chini Sanduku la Mungu, naye Abiathari akatoa dhabihu mpaka watu wote walipokuwa wameondoka mjini.

  17. 2 Samweli 15:25takriban 1021 KK

    Kisha mfalme akamwambia Sadoki, “Rudisha Sanduku la Mungu mjini. Ikiwa nitapata kibali mbele za Bwana, atanirudisha, nami nitaliona Sanduku hili tena pamoja na Maskani yake.

  18. 2 Samweli 15:26takriban 1021 KK

    Lakini kama yeye atasema, ‘Mimi sipendezwi nawe,’ basi mimi niko tayari; yeye na anifanye chochote aonacho chema kwake.”

  19. 2 Samweli 15:27takriban 1021 KK

    Pia mfalme alimwambia kuhani Sadoki, “Je, wewe si mwonaji? Rudi mjini kwa amani pamoja na mwanao Ahimaasi na Yonathani mwana wa Abiathari. Wewe na Abiathari wachukueni wana wenu wawili.

  20. 2 Samweli 15:28takriban 1021 KK

    Nitasubiri kwenye vivuko katika jangwa mpaka neno litakapotoka kwenu kuniarifu.”

  21. 2 Samweli 15:29takriban 1021 KK

    Kwa hiyo Sadoki na Abiathari wakarudisha Sanduku la Mungu mpaka Yerusalemu na kukaa huko.

  22. 2 Samweli 15:30takriban 1021 KK

    Bali Daudi akaendelea, akapanda Mlima wa Mizeituni, akaenda huku analia, akiwa amefunika kichwa chake na bila viatu miguuni. Watu wote waliokuwa pamoja naye nao wakafunika vichwa vyao, wakawa wanapanda mlima huku wanalia.

  23. 2 Samweli 15:31takriban 1021 KK

    Basi Daudi alikuwa ameambiwa, “Ahithofeli alikuwa miongoni mwa washiriki wa shauri baya la Absalomu.” Ndipo Daudi akaomba, akisema, “Ee Bwana, geuza shauri la Ahithofeli kuwa ujinga.”

  24. 2 Samweli 15:32takriban 1021 KK

    Daudi alipofika kwenye kilele cha mlima, mahali ambapo watu walikuwa wamezoea kumwabudu Mungu, Hushai, Mwariki, alikuwako huko kumlaki, joho lake likiwa limeraruka na mavumbi kichwani mwake.

  25. 2 Samweli 15:33takriban 1021 KK

    Daudi akamwambia, “Kama ukienda pamoja nami, utakuwa mzigo kwangu.