Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 7:29takriban 31 BK

    kwa sababu alifundisha kama yeye aliye na mamlaka, wala si kama walimu wao wa sheria.

  2. Mathayo 8:1takriban 31 BK

    Yesu aliposhuka kutoka mlimani, makutano makubwa ya watu yakamfuata.

  3. Mathayo 8:2takriban 31 BK

    Mtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake, akasema, “Bwana, kama ukitaka, unaweza kunitakasa.”

  4. Mathayo 8:3takriban 31 BK

    Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa yule mtu, akamwambia, “Nataka. Takasika!” Mara yule mtu akatakasika ukoma wake.

  5. Mathayo 8:4takriban 31 BK

    Kisha Yesu akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Mose, ili kuwa ushuhuda kwao.”

  6. Mathayo 8:5takriban 31 BK

    Yesu alipoingia Kapernaumu, jemadari mmoja alimjia, kumwomba msaada,

  7. Mathayo 8:6takriban 31 BK

    akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani na amepooza, tena ana maumivu makali ya kutisha.”

  8. Mathayo 8:7takriban 31 BK

    Yesu akamwambia, “Nitakuja na kumponya.”

  9. Mathayo 8:8takriban 31 BK

    Lakini yule jemadari akamwambia, “Bwana, mimi sistahili wewe kuingia chini ya dari yangu. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona.

  10. Mathayo 8:9takriban 31 BK

    Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu, ‘Nenda,’ yeye huenda; na mwingine nikimwambia, ‘Njoo,’ yeye huja. Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ yeye hufanya.”

  11. Mathayo 8:10takriban 31 BK

    Yesu aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata, “Amin, nawaambia, hata katika Israeli sijapata kuona yeyote mwenye imani kubwa namna hii.

  12. Mathayo 8:11takriban 31 BK

    Ninawaambia kwamba wengi watatoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Abrahamu, Isaki na Yakobo katika Ufalme wa Mbinguni.

  13. Mathayo 8:12takriban 31 BK

    Lakini warithi wa Ufalme watatupwa katika giza la nje, ambako kutakuwako kilio na kusaga meno.”

  14. Mathayo 8:13takriban 31 BK

    Kisha Yesu akamwambia yule jemadari, “Nenda na iwe kwako sawasawa na imani yako.” Naye yule mtumishi akapona saa ile ile.

  15. Mathayo 8:14takriban 31 BK

    Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wa Petro amelala kitandani, akiwa ana homa.

  16. Mathayo 8:15takriban 31 BK

    Akamgusa mkono wake na homa ikamwacha, naye akainuka na kuanza kumhudumia.

  17. Mathayo 8:16takriban 31 BK

    Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagawa na pepo wachafu, naye akawatoa wale pepo wachafu kwa neno lake, na kuwaponya wagonjwa wote.

  18. Mathayo 8:17takriban 31 BK

    Haya yalifanyika ili litimie lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kwamba: “Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu na alichukua magonjwa yetu.”

  19. Mathayo 8:18takriban 31 BK

    Yesu alipoona makutano mengi wamemzunguka, aliwaamuru wanafunzi wake wavuke mpaka ngʼambo ya ziwa.

  20. Mathayo 8:19takriban 31 BK

    Kisha mwalimu mmoja wa sheria akamjia Yesu na kumwambia, “Mwalimu, nitakufuata kokote uendako.”

  21. Mathayo 8:20takriban 31 BK

    Naye Yesu akamjibu, “Mbweha wana mapango, nao ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.”

  22. Mathayo 8:21takriban 31 BK

    Mwanafunzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.”

  23. Mathayo 8:22takriban 31 BK

    Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, uwaache wafu wawazike wafu wao.”

  24. Mathayo 8:23takriban 31 BK

    Naye alipoingia kwenye mashua, wanafunzi wake wakamfuata.

  25. Mathayo 8:24takriban 31 BK

    Ghafula, kukainuka dhoruba kali baharini hata mashua ikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Yesu alikuwa amelala usingizi.