Rukia maudhui

circa 6 BC – AD 30

The Life of Jesus

The eternal Son of God enters history: born in Bethlehem, baptized in the Jordan, crucified at Golgotha, raised on the third day.

3,779 mistari · 4 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Mathayo 7:4takriban 31 BK

    Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Acha nitoe kibanzi kwenye jicho lako,’ wakati kuna boriti kwenye jicho lako mwenyewe?

  2. Mathayo 7:5takriban 31 BK

    Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako.

  3. Mathayo 7:6takriban 31 BK

    “Msiwape mbwa vitu vilivyo vitakatifu; wala msitupie nguruwe lulu zenu. Kama mkifanya hivyo, watazikanyagakanyaga na kisha watawageukia na kuwararua vipande vipande.

  4. Mathayo 7:7takriban 31 BK

    “Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango.

  5. Mathayo 7:8takriban 31 BK

    Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango.

  6. Mathayo 7:9takriban 31 BK

    “Au ni nani miongoni mwenu ambaye mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe?

  7. Mathayo 7:10takriban 31 BK

    Au mwanawe akimwomba samaki atampa nyoka?

  8. Mathayo 7:11takriban 31 BK

    Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?

  9. Mathayo 7:12takriban 31 BK

    Kwa hiyo chochote mnachotaka mtendewe na watu, ninyi nanyi watendeeni vivyo hivyo. Kwa kuwa hii ndiyo Sheria na Manabii.

  10. Mathayo 7:13takriban 31 BK

    “Ingieni kupitia mlango mwembamba, kwa maana lango ni pana na njia ni pana ielekeayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa kupitia lango hilo.

  11. Mathayo 7:14takriban 31 BK

    Lakini mlango ni mwembamba na njia ni finyu ielekeayo kwenye uzima, nao ni wachache tu waionao.

  12. Mathayo 7:15takriban 31 BK

    “Jihadharini na manabii wa uongo, wanaowajia wakiwa wamevaa mavazi ya kondoo, lakini ndani ni mbwa mwitu wakali.

  13. Mathayo 7:16takriban 31 BK

    Mtawatambua kwa matunda yao. Je, watu huchuma zabibu kwenye miiba, au tini kwenye michongoma?

  14. Mathayo 7:17takriban 31 BK

    Vivyo hivyo, mti mwema huzaa matunda mazuri, na mti mbaya huzaa matunda mabaya.

  15. Mathayo 7:18takriban 31 BK

    Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri.

  16. Mathayo 7:19takriban 31 BK

    Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.

  17. Mathayo 7:20takriban 31 BK

    Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.

  18. Mathayo 7:21takriban 31 BK

    “Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni, bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

  19. Mathayo 7:22takriban 31 BK

    Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo wachafu na kufanya miujiza mingi?’

  20. Mathayo 7:23takriban 31 BK

    Ndipo nitakapowaambia wazi, ‘Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’

  21. Mathayo 7:24takriban 31 BK

    “Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba.

  22. Mathayo 7:25takriban 31 BK

    Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba. Lakini haikuanguka; kwa sababu msingi wake ulikuwa kwenye mwamba.

  23. Mathayo 7:26takriban 31 BK

    Naye kila anayesikia haya maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga.

  24. Mathayo 7:27takriban 31 BK

    Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, nao upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.”

  25. Mathayo 7:28takriban 31 BK

    Yesu alipomaliza kusema maneno haya, makutano ya watu wakashangazwa sana na mafundisho yake,