Rukia maudhui

circa 800–400 BC

The Hebrew Prophets

God speaks through Isaiah, Jeremiah, and the minor prophets—calling Israel to repentance and foretelling the coming Messiah.

3,706 mistari · 14 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Hosea 12:12takriban 725 KK

    Yakobo alikimbilia katika nchi ya Aramu; Israeli alitumika ili apate mke, ili aweze kulipa kwa ajili yake alichunga kondoo.

  2. Hosea 12:13takriban 725 KK

    Bwana alimtumia nabii kumpandisha Israeli kutoka Misri, kwa njia ya nabii alimtunza.

  3. Hosea 12:14takriban 725 KK

    Lakini Efraimu amemchochea sana hasira; Bwana wake ataleta juu yake hatia yake ya kumwaga damu naye atamlipiza kwa ajili ya dharau yake.

  4. Hosea 13:1takriban 725 KK

    Wakati Efraimu alipozungumza, watu walitetemeka, alikuwa ametukuzwa katika Israeli. Lakini alikuwa na hatia ya kumwabudu Baali naye akafa.

  5. Hosea 13:2takriban 725 KK

    Sasa wanatenda dhambi zaidi na zaidi; wanajitengenezea sanamu kutokana na fedha yao, vinyago vilivyotengenezwa kwa uhodari, vyote kazi ya fundi stadi. Inasemekana kuhusu hawa watu, “Hutoa dhabihu za binadamu na kubusu sanamu za ndama.”

  6. Hosea 13:3takriban 725 KK

    Kwa hiyo watakuwa kama ukungu wa asubuhi, kama umande wa alfajiri utowekao, kama makapi yapeperushwayo kutoka sakafu ya kupuria nafaka, kama moshi utorokao kupitia dirishani.

  7. Hosea 13:4takriban 725 KK

    “Bali mimi ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewaleta ninyi toka Misri. Msimkubali Mungu mwingine ila mimi, hakuna Mwokozi isipokuwa mimi.

  8. Hosea 13:5takriban 725 KK

    Niliwatunza huko jangwani, katika nchi yenye joto liunguzalo.

  9. Hosea 13:6takriban 725 KK

    Nilipowalisha, walishiba, waliposhiba, wakajivuna, kisha wakanisahau mimi.

  10. Hosea 13:7takriban 725 KK

    Kwa hiyo nitakuja juu yao kama simba, kama chui nitawavizia kando ya njia.

  11. Hosea 13:8takriban 725 KK

    Kama dubu aliyenyangʼanywa watoto wake, nitawashambulia na kurarua vifua vyenu. Kama simba nitawala; mnyama pori atawararua vipande vipande.

  12. Hosea 13:9takriban 725 KK

    “Ee Israeli, umeangamizwa, kwa sababu wewe u kinyume nami, kinyume na msaidizi wako.

  13. Hosea 13:10takriban 725 KK

    Yuko wapi mfalme wako, ili apate kukuokoa? Wako wapi watawala wako katika miji yako yote ambao ulisema kuwahusu, ‘Nipe mfalme na wakuu’?

  14. Hosea 13:11takriban 725 KK

    Hivyo katika hasira yangu nilikupa mfalme na katika ghadhabu yangu nilimwondoa.

  15. Hosea 13:12takriban 725 KK

    Kosa la Efraimu limehifadhiwa, dhambi zake zimewekwa katika kumbukumbu.

  16. Hosea 13:13takriban 725 KK

    Utungu kama wa mwanamke anayejifungua mtoto humjia, lakini yeye ni mtoto asiyekuwa na hekima; wakati utakapowadia hatatoka katika tumbo la mama yake.

  17. Hosea 13:14takriban 725 KK

    “Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi, nitawakomboa kutoka mautini. Yako wapi, ee mauti, mateso yako? Uko wapi, ee kuzimu, uharibifu wako? “Sitakuwa na huruma,

  18. Hosea 13:15takriban 725 KK

    hata ingawa Efraimu atastawi miongoni mwa ndugu zake. Upepo wa mashariki kutoka kwa Bwana utakuja, ukivuma kutoka jangwani, chemchemi yake haitatoa maji na kisima chake kitakauka. Ghala lake litatekwa hazina zake zote.

  19. Hosea 13:16takriban 725 KK

    Watu wa Samaria ni lazima wabebe hatia yao, kwa sababu wameasi dhidi ya Mungu wao. Wataanguka kwa upanga; watoto wao wadogo watatupwa kwa nguvu ardhini, wanawake wao walio na mimba watatumbuliwa.”

  20. Hosea 14:1takriban 725 KK

    Rudi, ee Israeli, kwa Bwana Mungu wako. Dhambi zako zimekuwa ndilo anguko lako!

  21. Hosea 14:2takriban 725 KK

    Chukueni maneno pamoja nanyi, mkamrudie Bwana. Mwambieni: “Samehe dhambi zetu zote na utupokee kwa neema, ili tuweze kutoa matunda yetu kama sadaka za mafahali.

  22. Hosea 14:3takriban 725 KK

    Ashuru hawezi kutuokoa, hatutapanda farasi wa vita. Kamwe hatutasema tena ‘Miungu yetu’ kwa kile ambacho mikono yetu wenyewe imetengeneza, kwa kuwa kwako wewe yatima hupata huruma.”

  23. Hosea 14:4takriban 725 KK

    “Nitaponya ukaidi wao na kuwapenda kwa hiari yangu, kwa kuwa hasira yangu imeondoka kwao.

  24. Hosea 14:5takriban 725 KK

    Nitakuwa kama umande kwa Israeli; atachanua kama yungiyungi. Kama mwerezi wa Lebanoni atashusha mizizi yake chini;

  25. Hosea 14:6takriban 725 KK

    matawi yake yatatanda. Fahari yake itakuwa kama mti wa mzeituni, harufu yake nzuri kama mwerezi wa Lebanoni.