Rukia maudhui

circa 800–400 BC

The Hebrew Prophets

God speaks through Isaiah, Jeremiah, and the minor prophets—calling Israel to repentance and foretelling the coming Messiah.

3,706 mistari · 14 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Yoeli 2:3takriban 800 KK

    Mbele yao moto unateketeza, nyuma yao miali ya moto inawaka kwa nguvu. Mbele yao nchi iko kama bustani ya Edeni, nyuma yao ni jangwa lisilofaa: hakuna kitu kinachowaepuka.

  2. Yoeli 2:4takriban 800 KK

    Wanaonekana kama farasi; wanakwenda mbio kama askari wapanda farasi.

  3. Yoeli 2:5takriban 800 KK

    Wanatoa sauti kama magari ya vita, wanaporukaruka juu ya vilele vya milima, kama mlio wa miali ya moto ilayo mabua, kama jeshi kubwa lililojipanga kwa ajili ya vita.

  4. Yoeli 2:6takriban 800 KK

    Wanapoonekana, mataifa yanakuwa katika maumivu makuu; kila uso unabadilika rangi.

  5. Yoeli 2:7takriban 800 KK

    Wanashambulia kama wapiganaji wa vita; wanapanda kuta kama askari. Wote wanatembea katika safu, hawapotoshi safu zao.

  6. Yoeli 2:8takriban 800 KK

    Hakuna anayemsukuma mwenzake; kila mmoja anakwenda mbele moja kwa moja. Wanapita katika vizuizi bila kuharibu safu zao.

  7. Yoeli 2:9takriban 800 KK

    Wanaenda kasi kuingia mjini; wanakimbia ukutani. Wanaingia ndani ya nyumba; kwa kuingilia madirishani kama wevi.

  8. Yoeli 2:10takriban 800 KK

    Mbele yao dunia inatikisika, anga linatetemeka, jua na mwezi vinatiwa giza, na nyota hazitoi mwanga wake tena.

  9. Yoeli 2:11takriban 800 KK

    Bwana anatoa mshindo wa ngurumo mbele ya jeshi lake; majeshi yake hayana idadi, ni wenye nguvu nyingi wale ambao hutii agizo lake. Siku ya Bwana ni kuu, ni ya kutisha. Ni nani anayeweza kuistahimili?

  10. Yoeli 2:12takriban 800 KK

    “Hata sasa,” asema Bwana, “nirudieni kwa mioyo yenu yote, kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza.”

  11. Yoeli 2:13takriban 800 KK

    Rarueni mioyo yenu na siyo mavazi yenu. Mrudieni Bwana, Mungu wenu, kwa maana yeye ndiye mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo, huona huruma, hujizuia kuleta maafa.

  12. Yoeli 2:14takriban 800 KK

    Ni nani ajuaye? Yeye aweza kugeuka na kuwa na huruma na kuacha baraka nyuma yake: sadaka za nafaka na sadaka za vinywaji kwa ajili ya Bwana Mungu wenu.

  13. Yoeli 2:15takriban 800 KK

    Pigeni tarumbeta katika Sayuni, tangazeni saumu takatifu, liiteni kusanyiko takatifu.

  14. Yoeli 2:16takriban 800 KK

    Wakusanyeni watu, wekeni wakfu kusanyiko; waleteni pamoja wazee, wakusanyeni watoto, wale wanyonyao maziwa. Bwana arusi na atoke chumbani mwake na bibi arusi naye atoke katika chumba chake.

  15. Yoeli 2:17takriban 800 KK

    Makuhani, ambao wanahudumu mbele za Bwana, na walie katikati ya ukumbi wa Hekalu na madhabahu. Waseme, “Wahurumie watu wako, Ee Bwana. Usifanye urithi wako kitu cha kudharauliwa, neno la dhihaka kati ya mataifa. Kwa nini wasemezane miongoni mwao, ‘Yuko wapi Mungu wao?’ ”

  16. Yoeli 2:18takriban 800 KK

    Kisha Bwana atakuwa na wivu kwa ajili ya nchi yake na kuwa na huruma juu ya watu wake.

  17. Yoeli 2:19takriban 800 KK

    Bwana atawajibu: “Ninawapelekea nafaka, mvinyo mpya na mafuta, vya kuwatosha ninyi hadi mridhike kabisa; kamwe sitawafanya tena kitu cha kudharauliwa na mataifa.

  18. Yoeli 2:20takriban 800 KK

    “Nitafukuza jeshi la kaskazini likae mbali nanyi, nikilisukuma ndani ya jangwa, askari wa safu za mbele wakienda ndani ya bahari ya mashariki na wale wa safu za nyuma katika bahari ya magharibi. Uvundo wake utapaa juu; harufu yake itapanda juu.” Hakika ametenda mambo makubwa.

  19. Yoeli 2:21takriban 800 KK

    Usiogope, ee nchi; furahi na kushangilia. Hakika Bwana ametenda mambo makubwa.

  20. Yoeli 2:22takriban 800 KK

    Msiogope, enyi wanyama pori, kwa kuwa mbuga za malisho yenu zinarudia ubichi. Miti nayo inazaa matunda, mtini na mzabibu inatoa utajiri wake.

  21. Yoeli 2:23takriban 800 KK

    Furahini, enyi watu wa Sayuni, shangilieni katika Bwana Mungu wenu, kwa kuwa amewapa mvua za vuli kwa kipimo cha haki. Anawapelekea mvua nyingi, mvua ya vuli na ya masika, kama mwanzoni.

  22. Yoeli 2:24takriban 800 KK

    Sakafu za kupuria zitajaa nafaka, mapipa yatafurika mvinyo mpya na mafuta.

  23. Yoeli 2:25takriban 800 KK

    “Nitawalipa kwa ajili ya miaka ile iliyoliwa na nzige: parare, madumadu na tunutu, jeshi langu kubwa ambalo nililituma katikati yenu.

  24. Yoeli 2:26takriban 800 KK

    Mtakuwa na wingi wa vyakula mpaka mshibe, na mtalisifu jina la Bwana Mungu wenu, ambaye amefanya maajabu kwa ajili yenu; kamwe watu wangu hawataaibishwa tena.

  25. Yoeli 2:27takriban 800 KK

    Ndipo mtakapojua kwamba mimi niko katika Israeli kwamba mimi ndimi Bwana Mungu wenu, na kwamba hakuna mwingine; kamwe watu wangu hawataaibika tena.