Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 2 Wakorintho 8:24takriban 60 BK

    Kwa hiyo waonyesheni wazi hawa ndugu uthibitisho wa upendo wenu na sababu inayotufanya tujivune kwa ajili yenu, mbele ya makanisa, ili yapate kuona.

  2. 2 Wakorintho 9:1takriban 60 BK

    Hakuna haja yangu kuwaandikia kuhusu huduma hii itolewayo kwa ajili ya watakatifu.

  3. 2 Wakorintho 9:2takriban 60 BK

    Kwa kuwa ninajua mlivyo na shauku ya kusaidia, nami nimekuwa nikijivuna kwa ajili ya jambo hilo kwa watu wa Makedonia, nikiwaambia kuwa ninyi wa Akaya mmekuwa tayari kutoa tangu mwaka jana na shauku yenu imewachochea wengi wao katika kutoa.

  4. 2 Wakorintho 9:3takriban 60 BK

    Lakini sasa nawatuma hawa ndugu ili kujivuna kwetu kuhusu mchango wenu kusiwe maneno matupu, bali mpate kuwa tayari kama nilivyosema mngekuwa tayari.

  5. 2 Wakorintho 9:4takriban 60 BK

    Kwa maana kama nikija na Mmakedonia yeyote na kuwakuta hamjawa tayari, tutaona aibu kusema chochote juu yenu katika matoleo.

  6. 2 Wakorintho 9:5takriban 60 BK

    Kwa hivyo niliona ni muhimu niwahimize hawa ndugu watangulie kuja huko kwenu kabla yangu, wafanye mipango ya hayo matoleo ya ukarimu mliyokuwa mmeahidi, ili yawe tayari kama matoleo ya hiari wala si kama ya kutozwa kwa nguvu.

  7. 2 Wakorintho 9:6takriban 60 BK

    Kumbukeni kwamba: Yeyote apandaye kwa uchache pia atavuna kwa uchache, naye apandaye kwa ukarimu pia atavuna kwa ukarimu.

  8. 2 Wakorintho 9:7takriban 60 BK

    Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.

  9. 2 Wakorintho 9:8takriban 60 BK

    Naye Mungu aweza kuwapa kila baraka kwa wingi, ili katika mambo yote kila wakati, mwe na kila kitu mnachohitaji, ili mweze kushiriki kwa wingi katika kila kazi njema.

  10. 2 Wakorintho 9:9takriban 60 BK

    Kama ilivyoandikwa: “Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini; haki yake hudumu milele.”

  11. 2 Wakorintho 9:10takriban 60 BK

    Yeye ampaye mpanzi mbegu kwa ajili ya kupanda na mkate kuwa chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu.

  12. 2 Wakorintho 9:11takriban 60 BK

    Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, na kupitia kwetu, ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani.

  13. 2 Wakorintho 9:12takriban 60 BK

    Huduma hii mnayofanya si tu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watakatifu, bali huzidi sana kwa shukrani nyingi apewazo Mungu.

  14. 2 Wakorintho 9:13takriban 60 BK

    Kwa sababu ya huduma ambayo mmejithibitisha wenyewe, watu watamtukuza Mungu kwa ajili ya utiifu ufuatanao na ukiri wenu wa Injili ya Kristo, na kwa ukarimu wenu wa kushiriki pamoja nao na pia wengine wote.

  15. 2 Wakorintho 9:14takriban 60 BK

    Nao katika maombi yao kwenu mioyo yao itawaonea shauku kwa sababu ya neema ipitayo kiasi mliyopewa na Mungu.

  16. 2 Wakorintho 9:15takriban 60 BK

    Ashukuriwe Mungu kwa karama yake isiyoelezeka.

  17. 2 Wakorintho 10:1takriban 60 BK

    Basi, mimi Paulo ninawasihi kwa unyenyekevu na upole wa Kristo, mimi niliye “mwoga” ninapokuwa pamoja nanyi ana kwa ana, lakini mwenye ujasiri nikiwa mbali nanyi!

  18. 2 Wakorintho 10:2takriban 60 BK

    Nawaomba nitakapokuja kwenu nisiwe na ujasiri dhidi ya watu fulani, kama ninavyotazamia kwa wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa kufuata namna ya ulimwengu huu.

  19. 2 Wakorintho 10:3takriban 60 BK

    Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo.

  20. 2 Wakorintho 10:4takriban 60 BK

    Silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome,

  21. 2 Wakorintho 10:5takriban 60 BK

    tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo,

  22. 2 Wakorintho 10:6takriban 60 BK

    tena tukiwa tayari kuadhibu kila tendo la kutotii, kutii kwenu kutakapokamilika.

  23. 2 Wakorintho 10:7takriban 60 BK

    Angalieni yale yaliyo machoni penu. Kama mtu yeyote anaamini kuwa yeye ni mali ya Kristo, basi kumbuka kuwa kama ulivyo wa Kristo, vivyo hivyo na sisi ndivyo tulivyo.

  24. 2 Wakorintho 10:8takriban 60 BK

    Basi hata kama nikijisifu zaidi kidogo kuhusu mamlaka tuliyo nayo, ambayo Bwana alitupa ili kuwajenga wala si kuwabomoa, mimi sitaionea haya.

  25. 2 Wakorintho 10:9takriban 60 BK

    Sitaki nionekane kama ninayejaribu kuwatisha kwa nyaraka zangu.