Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Warumi 11:22takriban 60 BK

    Angalia basi wema na ukali wa Mungu: Kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, kama utadumu katika wema wake. La sivyo, nawe utakatiliwa mbali.

  2. Warumi 11:23takriban 60 BK

    Wao nao wasipodumu katika kutokuamini kwao, watapandikizwa tena kwenye shina, kwa maana Mungu anao uwezo wa kuwapandikiza tena kwenye hilo shina.

  3. Warumi 11:24takriban 60 BK

    Ikiwa wewe ulikatwa kutoka kile ambacho kwa asili ni mzeituni mwitu na kupandikizwa kinyume cha asili kwenye mzeituni uliopandwa, si rahisi zaidi matawi haya ya asili kupandikizwa tena kwenye shina lake la mzeituni!

  4. Warumi 11:25takriban 60 BK

    Ndugu zangu, ili msije mkajidai kuwa wenye hekima kuliko mlivyo, nataka mfahamu siri hii: Ugumu umewapata Israeli kwa sehemu hadi idadi ya watu wa Mataifa watakaoingia itimie.

  5. Warumi 11:26takriban 60 BK

    Hivyo Israeli wote wataokolewa. Kama ilivyoandikwa: “Mkombozi atakuja kutoka Sayuni; ataondoa kutokumcha Mungu katika Yakobo.

  6. Warumi 11:27takriban 60 BK

    Hili ndilo agano langu nao nitakapoziondoa dhambi zao.”

  7. Warumi 11:28takriban 60 BK

    Kwa habari ya Injili, wao ni adui wa Mungu kwa ajili yenu, lakini kuhusu kule kuteuliwa kwao ni wapendwa, kwa ajili ya mababa zao wa zamani,

  8. Warumi 11:29takriban 60 BK

    kwa maana akishawapa watu karama, Mungu haziondoi, wala wito wake.

  9. Warumi 11:30takriban 60 BK

    Kama vile ninyi wakati fulani mlivyokuwa waasi kwa Mungu lakini sasa mmepata rehema kwa sababu ya kutokutii kwao,

  10. Warumi 11:31takriban 60 BK

    hivyo nao Waisraeli wamekuwa waasi ili kwamba wao nao sasa waweze kupata rehema kwa ajili ya rehema za Mungu kwenu.

  11. Warumi 11:32takriban 60 BK

    Kwa maana Mungu amewafunga wanadamu wote kwenye kuasi ili apate kuwarehemu wote.

  12. Warumi 11:33takriban 60 BK

    Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri wa hekima na maarifa ya Mungu! Tazama jinsi ambavyo hukumu zake hazichunguziki, na ambavyo njia zake zisivyotafutikana!

  13. Warumi 11:34takriban 60 BK

    “Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Bwana? Au ni nani ambaye amekuwa mshauri wake?”

  14. Warumi 11:35takriban 60 BK

    “Au ni nani aliyempa chochote ili arudishiwe?”

  15. Warumi 11:36takriban 60 BK

    Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake na kwa ajili yake. Utukufu ni wake milele! Amen.

  16. Warumi 12:1takriban 60 BK

    Kwa hiyo, ndugu zangu, nawasihi kwa rehema zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu na inayompendeza Mungu, hii ndiyo ibada yenu yenye maana.

  17. Warumi 12:2takriban 60 BK

    Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu.

  18. Warumi 12:3takriban 60 BK

    Kwa ajili ya neema niliyopewa nawaambia kila mmoja miongoni mwenu, asijidhanie kuwa bora kuliko impasavyo, bali afikiri kwa busara kwa kulingana na kipimo cha imani Mungu aliyompa.

  19. Warumi 12:4takriban 60 BK

    Kama vile katika mwili mmoja tulivyo na viungo vingi, navyo viungo vyote havina kazi moja,

  20. Warumi 12:5takriban 60 BK

    vivyo hivyo na sisi tulio wengi, tu mwili mmoja katika Kristo, nasi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.

  21. Warumi 12:6takriban 60 BK

    Tuna karama zilizotofautiana kila mmoja kutokana na neema tuliyopewa. Kama ni unabii na tutoe unabii kwa kadiri ya imani.

  22. Warumi 12:7takriban 60 BK

    Kama ni kuhudumu na tuhudumu, mwenye kufundisha na afundishe,

  23. Warumi 12:8takriban 60 BK

    kama ni kutia moyo na atie moyo, kama ni kuchangia kwa ajili ya mahitaji ya wengine na atoe kwa ukarimu, kama ni uongozi na aongoze kwa bidii, kama ni kuhurumia wengine na afanye hivyo kwa furaha.

  24. Warumi 12:9takriban 60 BK

    Upendo lazima usiwe na unafiki. Chukieni lililo ovu, shikamaneni na lililo jema.

  25. Warumi 12:10takriban 60 BK

    Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa ndugu. Waheshimuni na kuwatanguliza wengine.