Rukia maudhui

circa 1900–1700 BC

Jacob, Joseph & Egypt

Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.

840 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 26:26takriban 1804 KK

    Wakati huo, Abimeleki alikuwa amemjia kutoka Gerari, akifuatana na Ahuzathi mshauri wake, pamoja na Fikoli jemadari wa majeshi yake.

  2. Mwanzo 26:27takriban 1804 KK

    Isaki akawauliza, “Mbona mmekuja kwangu na ninyi mlinichukia na kunifukuza?”

  3. Mwanzo 26:28takriban 1804 KK

    Wakamjibu, “Tuliona wazi kuwa Bwana alikuwa pamoja nawe, kwa hiyo tukasema, ‘Inabidi kuwe na kiapo cha mapatano kati yetu, kati yetu na wewe. Na tufanye mkataba pamoja nawe

  4. Mwanzo 26:29takriban 1804 KK

    kwamba hutatudhuru, kama jinsi nasi hatukuwanyanyasa bali tuliwatendea mema wakati wote na kuwaondoa kwetu kwa amani. Tena sasa umebarikiwa na Bwana.’ ”

  5. Mwanzo 26:30takriban 1804 KK

    Basi Isaki akawaandalia karamu, nao wakala na kunywa.

  6. Mwanzo 26:31takriban 1804 KK

    Kesho yake asubuhi na mapema, wakaapizana wao kwa wao. Kisha Isaki akawaruhusu waende zao, wakamwacha Isaki kwa amani.

  7. Mwanzo 26:32takriban 1804 KK

    Siku hiyo watumishi wa Isaki wakaja wakampa habari kuhusu kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, “Tumepata maji!”

  8. Mwanzo 26:33takriban 1804 KK

    Naye akakiita Shiba, mpaka leo mji huo unaitwa Beer-Sheba.

  9. Mwanzo 26:34takriban 1796 KK

    Esau alipokuwa na umri wa miaka arobaini, akamwoa Yudithi binti Beeri Mhiti, kisha akamwoa Basemathi binti Eloni Mhiti.

  10. Mwanzo 26:35takriban 1796 KK

    Hawa walikuwa chanzo cha huzuni ya Isaki na Rebeka.

  11. Mwanzo 27:1takriban 1760 KK

    Isaki alipokuwa mzee na macho yake yalipokuwa yamekosa nguvu asiweze kuona tena, akamwita Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, “Mwanangu.” Akajibu, “Mimi hapa.”

  12. Mwanzo 27:2takriban 1760 KK

    Isaki akasema, “Mimi sasa ni mzee na sijui siku ya kifo changu.

  13. Mwanzo 27:3takriban 1760 KK

    Sasa basi, chukua silaha zako, podo na upinde, uende nyikani, ukawinde nyama pori kwa ajili yangu.

  14. Mwanzo 27:4takriban 1760 KK

    Uniandalie aina ya chakula kitamu nikipendacho uniletee nile, ili niweze kukubariki kabla sijafa.”

  15. Mwanzo 27:5takriban 1760 KK

    Basi Rebeka alikuwa akisikiliza Isaki alipokuwa akizungumza na mwanawe Esau. Esau alipoondoka kwenda nyikani kuwinda nyama pori na kuleta,

  16. Mwanzo 27:6takriban 1760 KK

    Rebeka akamwambia Yakobo mwanawe, “Tazama, nimemsikia baba yako akimwambia ndugu yako Esau,

  17. Mwanzo 27:7takriban 1760 KK

    ‘Niletee mawindo, kisha ukaniandalie chakula kitamu nile, ili niweze kukubariki mbele za Bwana kabla sijafa.’

  18. Mwanzo 27:8takriban 1760 KK

    Sasa, mwanangu, nisikilize kwa makini na ufanye yale ninayokuambia:

  19. Mwanzo 27:9takriban 1760 KK

    Nenda sasa katika kundi ukaniletee wana-mbuzi wawili wazuri, ili niandalie chakula kitamu kwa ajili ya baba yako, kama vile anavyopenda.

  20. Mwanzo 27:10takriban 1760 KK

    Kisha umpelekee baba yako ale, ili apate kukubariki kabla hajafa.”

  21. Mwanzo 27:11takriban 1760 KK

    Yakobo akamwambia Rebeka mama yake, “Lakini ndugu yangu Esau ana nywele mwilini, mimi nina ngozi nyororo.

  22. Mwanzo 27:12takriban 1760 KK

    Itakuwaje kama baba yangu akinigusa? Itaonekana kwake kama niliyemfanyia ujanja na kuleta laana juu yangu badala ya baraka.”

  23. Mwanzo 27:13takriban 1760 KK

    Mama yake akamwambia, “Mwanangu, laana na iwe juu yangu. Fanya tu ninalokuambia, nenda ukaniletee hao wana-mbuzi.”

  24. Mwanzo 27:14takriban 1760 KK

    Kwa hiyo alikwenda akawaleta, akampa mama yake, akaandaa chakula kitamu, kama vile alivyopenda baba yake.

  25. Mwanzo 27:15takriban 1760 KK

    Kisha Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau mwanawe wa kwanza, alizokuwa nazo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo.