Rukia maudhui

circa 1900–1700 BC

Jacob, Joseph & Egypt

Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.

840 mistari · 1 kitabu kimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

  1. Mwanzo 27:16takriban 1760 KK

    Pia akamfunika mikononi na sehemu laini ya shingo kwa ngozi za mbuzi.

  2. Mwanzo 27:17takriban 1760 KK

    Hatimaye akampa Yakobo hicho chakula kitamu pamoja na mkate aliouoka.

  3. Mwanzo 27:18takriban 1760 KK

    Akamwendea baba yake akasema, “Baba yangu.” Akajibu, “Naam, mwanangu, wewe ni nani?”

  4. Mwanzo 27:19takriban 1760 KK

    Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza. Nimefanya kama ulivyoniambia. Tafadhali uketi, ule sehemu ya mawindo yangu ili uweze kunibariki.”

  5. Mwanzo 27:20takriban 1760 KK

    Isaki akamuuliza mwanawe. “Umepataje haraka namna hii, mwanangu?” Akajibu, “Bwana Mungu wako amenifanikisha.”

  6. Mwanzo 27:21takriban 1760 KK

    Kisha Isaki akamwambia Yakobo, “Mwanangu tafadhali sogea karibu nami ili nikupapase, nione kama hakika ndiwe Esau mwanangu, au la.”

  7. Mwanzo 27:22takriban 1760 KK

    Yakobo akasogea karibu na baba yake Isaki, ambaye alimpapasa na kusema, “Sauti ni ya Yakobo, bali mikono ni ya Esau.”

  8. Mwanzo 27:23takriban 1760 KK

    Hakumtambua, kwa sababu mikono yake ilikuwa na nywele kama ya ndugu yake Esau, kwa hiyo akambariki.

  9. Mwanzo 27:24takriban 1760 KK

    Akamuuliza, “Hivi kweli wewe ni mwanangu Esau?” Akajibu, “Mimi ndiye.”

  10. Mwanzo 27:25takriban 1760 KK

    Kisha akasema, “Mwanangu, niletee sehemu ya mawindo yako nile, ili nipate kukubariki.” Yakobo akamletea naye akala, akamletea na divai akanywa.

  11. Mwanzo 27:26takriban 1760 KK

    Kisha Isaki baba yake akamwambia, “Njoo hapa, mwanangu, unibusu.”

  12. Mwanzo 27:27takriban 1760 KK

    Kwa hiyo akamwendea akambusu. Isaki aliposikia harufu ya nguo zake, akambariki, akasema, “Aha, harufu ya mwanangu ni kama harufu ya shamba ambalo Bwana amelibariki.

  13. Mwanzo 27:28takriban 1760 KK

    Mungu na akupe umande kutoka mbinguni na utajiri wa duniani: wingi wa nafaka na divai mpya.

  14. Mwanzo 27:29takriban 1760 KK

    Mataifa na yakutumikie na mataifa yakusujudie. Uwe bwana juu ya ndugu zako, na wana wa mama yako wakusujudie. Walaaniwe wale wakulaanio, nao wale wakubarikio wabarikiwe.”

  15. Mwanzo 27:30takriban 1760 KK

    Baada ya Isaki kumaliza kumbariki na baada tu ya Yakobo kuondoka kwa baba yake, ndugu yake Esau akaingia kutoka mawindoni.

  16. Mwanzo 27:31takriban 1760 KK

    Naye pia akaandaa chakula kitamu akamletea baba yake. Kisha akamwambia, “Baba yangu, keti ule sehemu ya mawindo yangu, ili upate kunibariki.”

  17. Mwanzo 27:32takriban 1760 KK

    Isaki baba yake akamuuliza, “Wewe ni nani?” Akajibu, “Mimi ni mwanao, mzaliwa wako wa kwanza, Esau.”

  18. Mwanzo 27:33takriban 1760 KK

    Isaki akatetemeka kwa nguvu sana, akasema, “Alikuwa nani basi, ambaye aliwinda mawindo akaniletea? Nilikula kabla tu hujaja na nikambariki, naye hakika atabarikiwa!”

  19. Mwanzo 27:34takriban 1760 KK

    Esau aliposikia maneno haya ya baba yake, akalia sauti kubwa na ya uchungu, na kumwambia baba yake, “Nibariki mimi, mimi pia, baba yangu!”

  20. Mwanzo 27:35takriban 1760 KK

    Lakini akasema, “Ndugu yako amekuja kwa udanganyifu na akachukua baraka yako.”

  21. Mwanzo 27:36takriban 1760 KK

    Esau akasema, “Si ndiyo sababu anaitwa Yakobo? Amenidanganya mara hizi mbili: Alichukua haki yangu ya kuzaliwa na sasa amechukua baraka yangu!” Kisha akauliza, “Hukubakiza hata baraka moja kwa ajili yangu?”

  22. Mwanzo 27:37takriban 1760 KK

    Isaki akamjibu Esau, “Nimemfanya yeye kuwa bwana juu yako, pia nimewafanya ndugu zako wote kuwa watumishi wake, nimemtegemeza kwa nafaka na divai mpya. Sasa nitaweza kukufanyia nini, mwanangu?”

  23. Mwanzo 27:38takriban 1760 KK

    Esau akamwambia baba yake, “Je, baba yangu una baraka moja tu? Unibariki mimi pia, baba yangu!” Kisha Esau akalia kwa sauti kubwa.

  24. Mwanzo 27:39takriban 1760 KK

    Baba yake Isaki akamjibu, akamwambia, “Makao yako yatakuwa mbali na utajiri wa dunia, mbali na umande wa mbinguni juu.

  25. Mwanzo 27:40takriban 1760 KK

    Utaishi kwa upanga, nawe utamtumikia ndugu yako, lakini wakati utakapokuwa umejikomboa, utatupa nira yake kutoka shingoni mwako.”