Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Righteousness

480 mistari · 132 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki, asemaye kweli toka moyoni mwake,

  2. na hana masingizio ulimini mwake, asiyemtenda jirani yake vibaya, na asiyemsingizia mwenzake,

  3. ambaye humdharau mtu mbaya, lakini huwaheshimu wale wamwogopao Bwana, yule atunzaye kiapo chake hata kama anaumia.

  4. Yeye akopeshaye fedha yake bila riba, na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia. Mtu afanyaye haya kamwe hatatikisika.

  5. Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao.

  6. Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.

  7. hunihuisha nafsi yangu. Huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

  8. Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana? Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?

  9. Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo.

  10. Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.

  11. Siri ya Bwana iko kwa wale wamchao, yeye huwajulisha agano lake.

  12. Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe, kwa maana kwa kiburi na dharau wao husema kwa majivuno dhidi ya wenye haki.

  13. Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.

  14. Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote.

  15. Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote,

  16. Ubaya utamuua mtu mwovu, nao adui za mwenye haki watahukumiwa.

  17. Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu, ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema.

  18. Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa au watoto wao wakiombaomba chakula.

  19. Watu waovu huvizia wenye haki, wakitafuta kuwaua;

  20. Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa, sikufunga mdomo wangu, Ee Bwana, kama ujuavyo.

  21. Ee Mungu, kiti chako cha enzi kitadumu milele na milele, fimbo ya utawala wa haki itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako.

  22. Unaipenda haki na kuchukia uovu; kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuweka juu ya wenzako, kwa kukupaka mafuta ya furaha.

  23. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.

  24. Hapo ndipo kutakapokuwa na dhabihu za haki, sadaka nzima za kuteketezwa za kukupendeza sana, pia mafahali watatolewa madhabahuni mwako.

  25. Unapenda mabaya kuliko mema, uongo kuliko kusema kweli.