Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Righteousness: Fruits of

298 mistari · 132 vipengele

Mistari kuhusu Fruits of

Chuja kwa kitabu
  1. Kama tukizitii kwa bidii amri hizi zote mbele za Bwana Mungu wetu, kama alivyotuamuru sisi, hiyo itakuwa haki yetu.”

  2. Naye Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, akawaambia Wareubeni, Wagadi na Manase, “Leo tunajua kwamba Bwana yuko pamoja nasi, kwa sababu hamkukosa uaminifu kwa Bwana katika jambo hili. Sasa mmewaokoa Waisraeli na mkono wa Bwana.”

  3. Mtu huyo ni kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao huzaa matunda kwa majira yake na majani yake hayanyauki. Lolote afanyalo hufanikiwa.

  4. Zaburi ya Daudi. Bwana, ni nani awezaye kukaa katika Hekalu lako? Nani awezaye kuishi katika mlima wako mtakatifu?

  5. Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki, asemaye kweli toka moyoni mwake,

  6. na hana masingizio ulimini mwake, asiyemtenda jirani yake vibaya, na asiyemsingizia mwenzake,

  7. ambaye humdharau mtu mbaya, lakini huwaheshimu wale wamwogopao Bwana, yule atunzaye kiapo chake hata kama anaumia.

  8. Yeye akopeshaye fedha yake bila riba, na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia. Mtu afanyaye haya kamwe hatatikisika.

  9. Nani awezaye kuupanda mlima wa Bwana? Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?

  10. Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo.

  11. Huyo atapokea baraka kutoka kwa Bwana, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.

  12. Sitaweka mbele ya macho yangu kitu kiovu. Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani; hawatashikamana nami.

  13. Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami; nitajitenga na kila ubaya.

  14. Heri wale wanaodumisha haki, ambao daima wanafanya yaliyo mema.

  15. Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu, yule mwenye rehema, huruma na haki.

  16. Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba, anayefanya mambo yake kwa haki.

  17. Hakika hatatikisika kamwe, mtu mwenye haki atakumbukwa milele.

  18. Hataogopa habari mbaya, moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana.

  19. Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu, mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake.

  20. ndipo utakapoelewa kumcha Bwana na kupata maarifa ya Mungu.

  21. Kwa maana Bwana hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.

  22. Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu, yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,

  23. kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki na kuhifadhi njia ya waaminifu wake.

  24. Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki na sawa: yaani kila njia nzuri.

  25. Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako, nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.