Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Prayer

720 mistari · 120 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kisha mtaniita, na mtakuja na kuniomba, nami nitawasikiliza.

  2. Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.

  3. Watakuja wakilia; wataomba wakati ninawarudisha. Nitawaongoza kando ya vijito vya maji katika mapito yaliyo tambarare ambapo hawatajikwaa, kwa sababu mimi ndimi baba wa Israeli, naye Efraimu ni mzaliwa wangu wa kwanza.

  4. ‘Niite nami nitakuitika na kukuambia mambo makuu na yasiyochunguzika, usiyoyajua.’

  5. Labda wataomba na kusihi mbele za Bwana na kila mmoja akageuka kutoka njia zake mbaya, kwa sababu hasira na ghadhabu zilizotamkwa dhidi ya watu hawa na Bwana ni kubwa.”

  6. Baada ya siku kumi, neno la Bwana likamjia Yeremia.

  7. “Bwana ni mwenye haki, hata hivyo niliasi dhidi ya amri yake. Sikilizeni, enyi mataifa yote, tazameni maumivu yangu. Wavulana wangu na wasichana wangu wamekwenda uhamishoni.

  8. “Uovu wao wote na uje mbele zako; uwashughulikie wao kama vile ulivyonishughulikia mimi kwa sababu ya dhambi zangu zote. Kulia kwangu kwa uchungu ni kwingi na moyo wangu umedhoofika.”

  9. Inuka, lia usiku, zamu za usiku zianzapo; mimina moyo wako kama maji mbele za Bwana. Mwinulie yeye mikono yako kwa ajili ya maisha ya watoto wako, ambao wanazimia kwa njaa kwenye kila mwanzo wa barabara.

  10. Bwana ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake, kwa yule ambaye humtafuta;

  11. Tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetu kwa Mungu mbinguni, na tuseme:

  12. “Tumetenda dhambi na kuasi nawe hujasamehe.

  13. Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yako kilio changu nikuombapo msaada.”

  14. Ulikuja karibu nilipokuita, nawe ukasema, “Usiogope.”

  15. Ee Bwana, ulichukua shauri langu, ukaukomboa uhai wangu.

  16. Umeona, Ee Bwana, ubaya niliotendewa. Tetea shauri langu!

  17. Umeona kina cha kisasi chao, mashauri yao yote mabaya dhidi yangu.

  18. Ee Bwana, umesikia matukano yao, mashauri yao yote mabaya dhidi yangu:

  19. kile adui zangu wanachonongʼona na kunungʼunikia dhidi yangu mchana kutwa.

  20. Watazame! Wakiwa wameketi au wamesimama, wananidhihaki katika nyimbo zao.

  21. Uwalipe kile wanachostahili, Ee Bwana, kwa yale ambayo mikono yao imetenda.

  22. Weka pazia juu ya mioyo yao, laana yako na iwe juu yao!

  23. Wafuatilie katika hasira na uwaangamize kutoka chini ya mbingu za Bwana.

  24. Taji imeanguka kutoka kichwani petu. Ole wetu, kwa maana tumetenda dhambi!

  25. “Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mara nyingine tena nitasikia maombi ya nyumba ya Israeli na kuwatendea jambo hili: Nitawafanya watu wake kuwa wengi kama kondoo,