Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Persecution

270 mistari · 61 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Usiwe mbali nami, kwa maana shida iko karibu na hakuna wa kunisaidia.

  2. Mafahali wengi wamenizunguka, mafahali wa Bashani wenye nguvu wamenizingira.

  3. Simba wangurumao wanaorarua mawindo yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu.

  4. Nimemiminwa kama maji, mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake. Moyo wangu umegeuka kuwa nta, umeyeyuka ndani yangu.

  5. Nguvu zangu zimekauka kama kigae, ulimi wangu umegandamana na kaakaa la kinywa changu, kwa sababu umenilaza katika mavumbi ya kifo.

  6. Mbwa wamenizunguka, kundi la watu waovu limenizingira, wametoboa mikono yangu na miguu yangu.

  7. Naweza kuhesabu mifupa yangu yote, watu wananikodolea macho na kunisimanga.

  8. Wanagawana nguo zangu wao kwa wao, na vazi langu wanalipigia kura.

  9. Lakini wewe, Ee Bwana, usiwe mbali. Ee Nguvu yangu, uje haraka unisaidie.

  10. Okoa maisha yangu na upanga, uhai wangu wa thamani kutoka nguvu za mbwa.

  11. Niokoe kutoka kinywani mwa simba, niokoe kutoka pembe za mafahali mwitu.

  12. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi.” Zaburi ya Daudi. Ee Mungu, niokoe, kwa maana maji yamenifika shingoni.

  13. Ninazama kwenye vilindi vya matope, pasipo mahali pa kukanyaga, Nimefika kwenye maji makuu, mafuriko yamenigharikisha.

  14. Nimechoka kwa kuomba msaada, koo langu limekauka. Macho yangu yanafifia, nikimtafuta Mungu wangu.

  15. Wale wanaonichukia bila sababu ni wengi kuliko nywele za kichwa changu; wengi ni adui kwangu bila sababu, wale wanaotafuta kuniangamiza. Ninalazimishwa kurudisha kitu ambacho sikuiba.

  16. Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu, wala hatia yangu haikufichika kwako.

  17. Ee Bwana, ewe Bwana Mwenye Nguvu Zote, wakutumainio wasiaibishwe kwa ajili yangu; wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.

  18. Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako, aibu imefunika uso wangu.

  19. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe.

  20. Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila, matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia.

  21. Ninapolia na kufunga, lazima nivumilie matusi.

  22. Ninapovaa nguo ya gunia, watu hunidharau.

  23. Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga, nimekuwa wimbo wa walevi.

  24. Lakini Ee Bwana, ninakuomba, kwa wakati ukupendezao; katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, unijibu kwa wokovu wako wa hakika.

  25. Uniokoe katika matope, usiniache nizame; niokoe na hao wanichukiao, kutoka kwenye vilindi vya maji.