Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Persecution

270 mistari · 61 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na wake, yeye atakuponda kichwa, nawe utamuuma kisigino.”

  2. Kisha mfalme mpya ambaye hakufahamu habari za Yosefu akatawala Misri.

  3. Akawaambia watu wake, “Tazameni, Waisraeli wamekuwa wengi mno kwa idadi kutuliko sisi.

  4. Njooni, ni lazima tuwashughulikie kwa uangalifu, la sivyo watazidi kuwa wengi zaidi, na ikiwa patatokea vita, watajiunga na adui zetu kupigana dhidi yetu na kuondoka katika nchi hii.”

  5. Basi Wamisri wakaweka wasimamizi wa kuwasimamia na kuwatesa Waisraeli kwa kazi ngumu, nao wakajenga miji ya Pithomu na Ramesesi ya kuweka akiba ya Farao.

  6. Lakini walivyozidi kuteswa ndivyo walivyozidi kuongezeka na kuenea katika nchi; Wamisri wakawaogopa Waisraeli,

  7. kwa hiyo wakawatumikisha kwa ukatili.

  8. Wakafanya maisha ya Waisraeli kuwa machungu kwa kufanya kazi ngumu ya kutengeneza lami na kufyatua matofali, na kazi zote za mashambani; katika kazi zao zote ngumu, Wamisri waliwatumia Waisraeli kwa ukatili.

  9. Pia akaongeza, “Kwa nini bwana wangu anamfuatia mtumishi wake? Nimefanya nini, nalo kosa langu ni lipi nililolifanya niwe na hatia?

  10. Hivyo Yezebeli akamtuma mjumbe kwa Eliya, kusema, “Hao miungu initendee hivyo na kuzidi, kama kufikia kesho wakati kama huu sitaifanya roho yako kama mmojawapo wa hao manabii.”

  11. Mkaseme, ‘Hivi ndivyo asemavyo mfalme: Mwekeni mtu huyu gerezani na asipewe chochote ila mkate na maji mpaka nitakaporudi salama.’ ”

  12. Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na kabila za watu kula njama bure?

  13. Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya Bwana na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.

  14. Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”

  15. Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau.

  16. Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,

  17. Ombolezo la Daudi kwa Bwana kwa sababu ya Kushi, Mbenyamini. Ee Bwana, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe, uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia,

  18. Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto.

  19. Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.

  20. Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.

  21. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Kulungu wa Alfajiri.” Zaburi ya Daudi. Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kwa nini uko mbali hivyo kuniokoa? Mbali hivyo na maneno ya kuugua kwangu?

  22. Ee Mungu wangu, ninalia mchana, lakini hunijibu, hata usiku, sinyamazi.

  23. Mimi ni mnyoo wala si mwanadamu, wanaume wamenibeza, na watu wamenidharau.

  24. Wote wanionao hunidhihaki, hunivurumishia matusi, wakitikisa vichwa vyao:

  25. Husema, “Anamtegemea Bwana, basi Bwana na amwokoe. Amkomboe basi, kwa maana anapendezwa naye.”