Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Judgments

271 mistari · 91 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha Bwana,

  2. kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu,

  3. watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao.

  4. Ee nyumba ya Israeli,” asema Bwana, “Ninaleta taifa toka mbali dhidi yako, taifa la kale na linaloendelea kudumu, taifa ambalo lugha yao huijui, wala msemo wao huwezi kuuelewa.

  5. Podo zao ni kama kaburi lililo wazi, wote ni mashujaa hodari wa vita.

  6. Watayaangamiza mazao yenu na chakula chenu, wataangamiza wana wenu na mabinti zenu; wataangamiza makundi yenu ya kondoo na ya ngʼombe, wataangamiza mizabibu yenu na mitini yenu. Kwa upanga wataangamiza miji yenye maboma mliyoitumainia.

  7. “Hata hivyo katika siku hizo, sitakuangamiza kabisa,” asema Bwana.

  8. Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, “Sikiliza Hanania! Bwana hajakutuma, lakini wewe umelishawishi taifa hili kuamini uongo.

  9. Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana: ‘Hivi karibuni nitakuondoa kutoka juu ya uso wa dunia. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi ya Bwana.’ ”

  10. Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa.

  11. Tena na tena, niliwatuma watumishi wangu manabii ambao walisema, ‘Msifanye jambo hili la kuchukiza ambalo nalichukia!’

  12. Lakini hawakusikiliza wala hawakujali, hawakugeuka ili kuuacha uovu wao, wala hawakuacha kufukiza uvumba kwa miungu mingine.

  13. Kwa hiyo hasira yangu kali ilimwagika, ikawaka dhidi ya miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu, na kuifanya ukiwa na magofu kama ilivyo leo.

  14. Mimi ndiye mtu aliyeona mateso kwa fimbo ya ghadhabu yake.

  15. Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee gizani wala si katika nuru;

  16. hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu tena na tena, mchana kutwa.

  17. Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa na ameivunja mifupa yangu.

  18. Amenizingira na kunizunguka kwa uchungu na taabu.

  19. Amenifanya niishi gizani kama wale waliokufa.

  20. Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka, amenifunga kwa minyororo mizito.

  21. Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada, anakataa kupokea maombi yangu.

  22. Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe, amepotosha njia zangu.

  23. Kama dubu aviziaye, kama simba mafichoni,

  24. ameniburuta kutoka njia, akanirarua na kuniacha bila msaada.

  25. Amevuta upinde wake na kunifanya mimi niwe lengo kwa ajili ya mishale yake.