Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Judgments: Despising the warnings of God

11 mistari · 91 vipengele

Mistari kuhusu Despising the warnings of God

  1. Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita na hakuna yeyote aliyekubali niliponyoosha mkono wangu,

  2. kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote na hamkukubali karipio langu,

  3. mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, nitawadhihaki wakati janga litawapata:

  4. wakati janga litawapata kama tufani, wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli, wakati dhiki na taabu zitawalemea.

  5. “Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu; watanitafuta lakini hawatanipata.

  6. Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha Bwana,

  7. kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu,

  8. watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao.

  9. Tena na tena, niliwatuma watumishi wangu manabii ambao walisema, ‘Msifanye jambo hili la kuchukiza ambalo nalichukia!’

  10. Lakini hawakusikiliza wala hawakujali, hawakugeuka ili kuuacha uovu wao, wala hawakuacha kufukiza uvumba kwa miungu mingine.

  11. Kwa hiyo hasira yangu kali ilimwagika, ikawaka dhidi ya miji ya Yuda na barabara za Yerusalemu, na kuifanya ukiwa na magofu kama ilivyo leo.