Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu God

662 mistari · 46 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Kama nikiinua kichwa changu juu, unaninyatia kama simba, na kuonyesha tena uwezo wa kutisha dhidi yangu.

  2. Wewe waleta mashahidi wapya dhidi yangu na kuzidisha hasira yako juu yangu; nazo nguvu zako zinanijia wimbi moja baada ya jingine.

  3. “Kwa nini basi ulinitoa tumboni? Ninatamani ningekufa kabla jicho lolote halijaniona.

  4. “Lakini ulizeni wanyama, nao watawafundisha, au ndege wa angani, nao watawaambia;

  5. au zungumzeni na dunia, nayo itawafundisha, au acheni samaki wa baharini wawape taarifa.

  6. Ni nani miongoni mwa hawa wote asiyejua kwamba mkono wa Bwana ndio uliofanya hili?

  7. Mkononi mwake kuna uhai wa kila kiumbe, na pumzi ya wanadamu wote.

  8. Je, sikio haliyajaribu maneno kama vile ulimi uonjavyo chakula?

  9. Je, hekima haipatikani katikati ya wazee? Je, maisha marefu hayaleti ufahamu?

  10. “Hekima na nguvu ni vya Mungu; shauri na ufahamu ni vyake yeye.

  11. Kile anachokibomoa hakiwezi kujengeka tena; mtu aliyefungiwa naye hawezi kufunguliwa.

  12. Akizuia maji, huwa pana ukame; akiyaachia maji, huharibu nchi.

  13. Kwake kuna nguvu na ushindi; adanganywaye na adanganyaye, wote wawili ni wake.

  14. Yeye huwaondoa washauri wakiwa wametekwa nyara, naye huwapumbaza wanaotoa maamuzi.

  15. Huondoa pingu zilizofungwa na wafalme, na kuwafunga mishipi ya kiunoni.

  16. Huwaondoa makuhani wakiwa wametekwa nyara, na kuwaangusha waliojiimarisha muda mrefu.

  17. Hunyamazisha midomo ya washauri wanaoaminika, na kuondoa busara ya wazee.

  18. Hutandaza anga la kaskazini mahali patupu; naye huiningʼiniza dunia mahali pasipo na kitu.

  19. Huyafungia maji kwenye mawingu yake, hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.

  20. Huufunika uso wa mwezi mpevu, akitandaza mawingu juu yake.

  21. Amechora mstari wa upeo juu ya uso wa maji, ameweka mpaka wa nuru na giza.

  22. Nguzo za mbingu nazo zatetemeka, zinatishika anapozikemea.

  23. Kwa nguvu zake aliisukasuka bahari; kwa hekima yake alimkata Rahabu vipande vipande.

  24. Aliisafisha anga kwa pumzi yake; kwa mkono wake alimchoma joka aendaye mbio.

  25. Haya ni mambo madogo tu katika matendo yake; tazama jinsi ulivyo mdogo mnongʼono tunaousikia kumhusu! Ni nani basi awezaye kuelewa ngurumo za nguvu zake?”