Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu God

662 mistari · 46 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. “Siku zangu zapita mbio kuliko mkimbiaji; zinapita upesi bila kuona furaha hata kidogo.

  2. Zinapita upesi kama mashua ya mafunjo, mfano wa tai ayashukiaye mawindo kwa ghafula.

  3. Kama nikisema, ‘Nitayasahau malalamiko yangu, nitabadili sura ya uso wangu na kutabasamu,’

  4. bado ninahofia mateso yangu yote, kwa kuwa ninajua hutanihesabu kuwa sina hatia.

  5. Kwa kuwa nimeonekana mwenye hatia, kwa nini basi nitaabishwe bure?

  6. Hata kama ningejiosha kwa sabuni na kutakasa mikono yangu kwa magadi,

  7. wewe ungenitupa kwenye shimo la utelezi kiasi kwamba hata nguo zangu zingenichukia sana.

  8. “Yeye si mwanadamu kama mimi ili niweze kumjibu, ili kwamba tuweze kushindana naye mahakamani.

  9. Laiti angelikuwepo mtu wa kutupatanisha kati yetu, aweke mkono wake juu yetu sote wawili,

  10. mtu angeliiondoa fimbo ya Mungu juu yangu, ili utisho wake usiendelee kunitia hofu.

  11. Ndipo ningenena naye, bila kumwogopa, lakini kama ilivyo kwangu sasa, sitaweza.

  12. Nitamwambia Mungu: Usinihukumu, bali niambie una mashtaka gani dhidi yangu.

  13. Je, inakupendeza wewe kunionea, kuikataa kwa dharau kazi ya mikono yako, huku wewe ukitabasamu juu ya mipango ya waovu?

  14. Je, wewe una macho ya kimwili? Je, wewe huona kama mwanadamu aonavyo?

  15. Je, siku zako ni kama zile za mwanadamu, au miaka yako ni kama ile ya mtu,

  16. ili kwamba utafute makosa yangu na kuichunguza dhambi yangu;

  17. ingawa wajua kuwa mimi sina hatia, na hakuna awezaye kunitoa mkononi mwako?

  18. “Mikono yako ndiyo iliyoniumba na kunifanya. Je, sasa utageuka na kuniangamiza?

  19. Kumbuka kuwa ulinifinyanga kama udongo wa mfinyanzi. Je, sasa utanifanya kuwa mavumbi tena?

  20. Je, wewe hukunimimina mimi kama maziwa, na kunigandisha kama jibini,

  21. ukanivika ngozi na nyama, na kuniunga pamoja kwa mifupa na mishipa?

  22. Umenipa uhai na kunitendea wema, katika uangalizi wako umeilinda roho yangu.

  23. “Lakini hili ndilo ulilolificha moyoni mwako, nami ninajua kuwa hili lilikuwa katika nia yako:

  24. Kama nilifanya dhambi, ungekuwa umeniona, wala usingeacha kosa langu lipite bila kuadhibiwa.

  25. Kama nina hatia, ole wangu! Hata kama ningekuwa sina hatia, siwezi kukiinua kichwa changu, kwa kuwa nimejawa na aibu, na kuzama katika mateso yangu.