Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Genealogy

114 mistari · 8 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Tera alipokuwa bado hai, Harani akafa huko Uru ya Wakaldayo, nchi alimozaliwa.

  2. Abramu na Nahori walioa. Mke wa Abramu aliitwa Sarai, na mke wa Nahori aliitwa Milka; Milka na Iska walikuwa watoto wa Harani.

  3. Sarai alikuwa tasa, hakuwa na watoto.

  4. Tera akamchukua Abramu mwanawe, Loti mwana wa Harani mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka kwa pamoja katika Uru ya Wakaldayo kwenda nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani, wakaishi huko.

  5. Tera alikufa huko Harani akiwa na miaka 205.

  6. Hivi ndivyo vizazi vya Peresi: Peresi alimzaa Hesroni,

  7. Hesroni akamzaa Ramu, Ramu akamzaa Aminadabu,

  8. Aminadabu akamzaa Nashoni, Nashoni akamzaa Salmoni,

  9. Salmoni akamzaa Boazi, Boazi akamzaa Obedi,

  10. Obedi akamzaa Yese, na Yese akamzaa Daudi.

  11. Adamu, Sethi, Enoshi,

  12. Kenani, Mahalaleli, Yaredi,

  13. Enoki, Methusela, Lameki, Noa.

  14. Wana wa Noa walikuwa: Shemu, Hamu na Yafethi.

  15. Wana wa Yafethi walikuwa: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi.

  16. Wana wa Gomeri walikuwa: Ashkenazi, Rifathi na Togarma.

  17. Wana wa Yavani walikuwa: Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu.

  18. Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misraimu, Putu na Kanaani.

  19. Wana wa Kushi walikuwa: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa: Sheba na Dedani.

  20. Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua akawa mtu shujaa katika nchi.

  21. Misraimu akawazaa: Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,

  22. Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori.

  23. Wana wa Kanaani walikuwa: Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi,

  24. Wayebusi, Waamori, Wagirgashi,

  25. Wahivi, Waariki, Wasini,