Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu Genealogy

114 mistari · 8 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. wa wazao wa Yoabu, alikuwa Obadia mwana wa Yehieli na wanaume 218 pamoja naye;

  2. wa wazao wa Bani, alikuwa Shelomithi mwana wa Yosifia na wanaume 160 pamoja naye;

  3. wa wazao wa Bebai, alikuwa Zekaria mwana wa Bebai na wanaume 28 pamoja naye;

  4. wa wazao wa Azgadi, alikuwa Yohanani mwana wa Hakatani na wanaume 110 pamoja naye;

  5. wa wazao wa Adonikamu, hawa walikuwa wa mwisho ambao majina yao ni Elifeleti, Yeueli, Shemaya na wanaume 60 pamoja nao;

  6. wa wazao wa Bigwai, walikuwa Uthai na Zakuri na wanaume 70 pamoja nao.

  7. Niliwakusanya kwenye mto utiririkao kuelekea Ahava, nasi tukapiga kambi pale siku tatu. Wakati nilipokagua kati ya watu na makuhani, sikuwapata Walawi.

  8. Habari za ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu:

  9. Abrahamu akamzaa Isaki, Isaki akamzaa Yakobo, Yakobo akawazaa Yuda na ndugu zake,

  10. Yuda akawazaa Peresi na Zera, ambao mama yao alikuwa Tamari, Peresi akamzaa Hesroni, Hesroni akamzaa Aramu,

  11. Aramu akamzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nashoni, Nashoni akamzaa Salmoni,

  12. Salmoni akamzaa Boazi, na mama yake Boazi alikuwa Rahabu, Boazi akamzaa Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruthu, Obedi akamzaa Yese,

  13. Yese akamzaa Daudi ambaye alikuwa mfalme. Daudi akamzaa Solomoni, ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria.

  14. Solomoni akamzaa Rehoboamu, Rehoboamu akamzaa Abiya, Abiya akamzaa Asa,

  15. Asa akamzaa Yehoshafati, Yehoshafati akamzaa Yoramu, Yoramu akamzaa Uzia,

  16. Uzia akamzaa Yothamu, Yothamu akamzaa Ahazi, Ahazi akamzaa Hezekia,

  17. Hezekia akamzaa Manase, Manase akamzaa Amoni, Amoni akamzaa Yosia,

  18. wakati wa uhamisho wa Babeli, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake.

  19. Baada ya uhamisho wa Babeli: Yekonia alimzaa Shealtieli, Shealtieli akamzaa Zerubabeli,

  20. Zerubabeli akamzaa Abiudi, Abiudi akamzaa Eliakimu, Eliakimu akamzaa Azori,

  21. Azori akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Akimu, Akimu akamzaa Eliudi,

  22. Eliudi akamzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Matani, Matani akamzaa Yakobo,

  23. naye Yakobo akamzaa Yosefu ambaye alikuwa mumewe Maria, mama yake Yesu, aitwaye Kristo.

  24. Yesu alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza huduma yake. Alikuwa akidhaniwa kuwa mwana wa Yosefu, Yosefu alikuwa mwana wa Eli,

  25. Eli alikuwa mwana wa Mathati, Mathati alikuwa mwana wa Lawi, Lawi alikuwa mwana wa Melki, Melki alikuwa mwana wa Yanai, Yanai alikuwa mwana wa Yosefu,