Rukia maudhui

circa 970–930 BC

Solomon & The Temple

Solomon builds the great Temple in Jerusalem and rules with unprecedented wisdom and wealth before foreign gods divide his heart.

635 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 2 Nyakati 4:15takriban 1011 KK

    hiyo Bahari na hao mafahali kumi na wawili chini yake;

  2. 2 Nyakati 4:16takriban 1011 KK

    pia hayo masufuria, masepetu, uma za nyama na vyombo vingine vyote vilivyohusiana. Vitu vyote ambavyo Huramu-Abi alimtengenezea Mfalme Solomoni kwa ajili ya Hekalu la Bwana vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa.

  3. 2 Nyakati 4:17takriban 1011 KK

    Mfalme aliagiza wavisubu vitu hivi kwenye kalibu za udongo wa mfinyanzi katika uwanda wa Yordani kati ya Sukothi na Sereda.

  4. 2 Nyakati 4:18takriban 1011 KK

    Vitu hivi vyote Mfalme Solomoni alivyotengeneza vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzito wa shaba haungekadirika.

  5. 2 Nyakati 4:19takriban 1011 KK

    Solomoni pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mungu: madhabahu ya dhahabu; meza za kuweka mikate ya Wonyesho;

  6. 2 Nyakati 4:20takriban 1011 KK

    vinara vya taa vya dhahabu safi pamoja na taa zake ili ziwake mbele ya sehemu takatifu ya ndani kama ilivyoelekezwa;

  7. 2 Nyakati 4:21takriban 1011 KK

    maua ya dhahabu yaliyofanyizwa, taa na makoleo (vilikuwa vya dhahabu bora kabisa);

  8. 2 Nyakati 4:22takriban 1011 KK

    mikasi ya dhahabu safi, mabakuli ya kunyunyizia, masinia na vyetezo; milango ya dhahabu ya Hekalu: yaani milango ya ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, na milango ya ukumbi mkuu.

  9. 2 Nyakati 5:1takriban 1004 KK

    Hivyo Solomoni alipomaliza kazi ya Hekalu la Bwana, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: yaani, fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la Mungu.

  10. 2 Nyakati 5:2takriban 1004 KK

    Kisha Solomoni akawaita huko Yerusalemu wazee wa Israeli, viongozi wote wa makabila na wakuu wa jamaa za Waisraeli, ili walilete Sanduku la Agano la Bwana kutoka Sayuni, Mji wa Daudi.

  11. 2 Nyakati 5:3takriban 1004 KK

    Nao wanaume wote wa Israeli wakakusanyika kwa mfalme wakati wa sikukuu mwezi wa saba.

  12. 2 Nyakati 5:4takriban 1004 KK

    Wazee wote wa Israeli walipofika, Walawi wakajitwika Sanduku la Agano,

  13. 2 Nyakati 5:5takriban 1004 KK

    nao wakalipandisha Sanduku na Hema la Kukutania pamoja na vyombo vyote vitakatifu vilivyokuwa ndani yake. Makuhani, waliokuwa Walawi, walivibeba vitu hivyo,

  14. 2 Nyakati 5:6takriban 1004 KK

    naye Mfalme Solomoni na kusanyiko lote la Israeli waliokusanyika kumzunguka walikuwa mbele ya hilo Sanduku, nao wakatoa dhabihu nyingi za kondoo na ngʼombe ambao idadi yao haikuwezekana kuandikwa au kuhesabiwa.

  15. 2 Nyakati 5:7takriban 1004 KK

    Makuhani wakalileta Sanduku la Agano la Bwana hadi mahali pake ndani ya sehemu takatifu ndani ya Hekalu, yaani Patakatifu pa Patakatifu, na kuliweka chini ya mabawa ya makerubi.

  16. 2 Nyakati 5:8takriban 1004 KK

    Makerubi yalitandaza mabawa yao juu ya mahali pa Sanduku la Agano na kufunika Sanduku na mipiko yake ya kubebea.

  17. 2 Nyakati 5:9takriban 1004 KK

    Mipiko hiyo ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba ncha zake zilizojitokeza kutoka kwenye Sanduku, nazo zilionekana ukiwa mbele ya Patakatifu pa Patakatifu, lakini sio nje ya Mahali Patakatifu. Hiyo mipiko ipo hata leo.

  18. 2 Nyakati 5:10takriban 1004 KK

    Ndani ya Sanduku hapakuwepo kitu kingine chochote isipokuwa zile mbao mbili ambazo Mose alikuwa ameziweka ndani yake huko Horebu, mahali ambapo Bwana alifanya Agano na Waisraeli baada ya kutoka Misri.

  19. 2 Nyakati 5:11takriban 1004 KK

    Basi makuhani wakaondoka hapo Mahali Patakatifu. Makuhani wote waliokuwa huko walikuwa wamejiweka wakfu, bila kujali migawanyo yao.

  20. 2 Nyakati 5:12takriban 1004 KK

    Walawi wote waliokuwa waimbaji, yaani, Asafu, Hemani, Yeduthuni, wana wa ndugu zao, walisimama upande wa mashariki wa madhabahu, wakiwa wamevaa kitani safi huku wakipiga matoazi, vinubi na zeze. Walikuwa pamoja na makuhani 120 wakipiga tarumbeta.

  21. 2 Nyakati 5:13takriban 1004 KK

    Wapiga tarumbeta na waimbaji wakaungana katika sauti linganifu, ikawa kama vile ni sauti moja, wakimsifu na kumshukuru Bwana, nao alipoinua sauti zao pamoja na tarumbeta na matoazi na vyombo vingine vya uimbaji, wakamsifu Bwana wakisema: “Yeye ni mwema; upendo wake unadumu milele.” Ndipo Hekalu la Bwana likajazwa na wingu,

  22. 2 Nyakati 5:14takriban 1004 KK

    nao makuhani hawakuweza kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu, kwa kuwa utukufu wa Bwana ulijaza Hekalu la Mungu.

  23. 2 Nyakati 6:1takriban 1004 KK

    Ndipo Solomoni akasema, “Bwana alisema kwamba ataishi katika giza nene.

  24. 2 Nyakati 6:2takriban 1004 KK

    Nimejenga Hekalu zuri kwa ajili yako, mahali pako pa kukaa milele.”

  25. 2 Nyakati 6:3takriban 1004 KK

    Kusanyiko lote la Israeli lilipokuwa limesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki.