Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kutoka 22:10takriban 1491 KK

    “Kama mtu akimpa jirani yake punda, ngʼombe, kondoo au mnyama mwingine yeyote amtunzie, akifa au akijeruhiwa au akichukuliwa wakati haonekani na mtu yeyote,

  2. Kutoka 22:11takriban 1491 KK

    jambo hili kati yao wawili litaamuliwa kwa kuapa kiapo mbele za Bwana, kwamba huyo jirani hakuhusika na wizi wa mali ya jirani yake. Mwenye mali itampasa akubali jambo hili, na hakuna malipo yatakayohitajika.

  3. Kutoka 22:12takriban 1491 KK

    Lakini kama mnyama aliibwa kwa jirani, itampasa amlipe mwenye mnyama.

  4. Kutoka 22:13takriban 1491 KK

    Kama ameraruliwa na mnyama pori, ataleta mabaki ya mnyama kama ushahidi, naye hatadaiwa kulipa mnyama aliyeraruliwa.

  5. Kutoka 22:14takriban 1491 KK

    “Kama mtu akimwazima mnyama kutoka kwa jirani yake, na kama akiumia au akafa na mwenye mnyama hayupo, lazima amlipe huyo mnyama.

  6. Kutoka 22:15takriban 1491 KK

    Lakini mwenye mnyama akiwa angalipo na mnyama wake, mwazimaji hatalazimika kumlipa. Kama mnyama alikuwa amekodishwa, fedha iliyolipwa kwa kukodisha inatosha kwa kufidia hasara.

  7. Kutoka 22:16takriban 1491 KK

    “Kama mtu akimshawishi bikira ambaye hajaposwa na akilala naye, lazima alipe mahari, kisha atamwoa msichana huyo.

  8. Kutoka 22:17takriban 1491 KK

    Baba wa msichana akikataa katakata kumpa huyo mtu huyo msichana wake, bado ni lazima huyo mtu atalipa mahari kama inavyostahili malipo ya ubikira.

  9. Kutoka 22:18takriban 1491 KK

    “Usiruhusu mwanamke mchawi aishi.

  10. Kutoka 22:19takriban 1491 KK

    “Mtu yeyote aziniye na mnyama lazima auawe.

  11. Kutoka 22:20takriban 1491 KK

    “Mtu awaye yote anayemtolea mungu mwingine dhabihu isipokuwa Bwana, lazima aangamizwe.

  12. Kutoka 22:21takriban 1491 KK

    “Usimtendee mgeni vibaya au kumwonea, kwa kuwa nanyi mlikuwa wageni huko Misri.

  13. Kutoka 22:22takriban 1491 KK

    “Usimdhulumu mjane wala yatima.

  14. Kutoka 22:23takriban 1491 KK

    Kama ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao.

  15. Kutoka 22:24takriban 1491 KK

    Hasira yangu itawaka, nami nitawaua kwa upanga, wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu watakuwa yatima.

  16. Kutoka 22:25takriban 1491 KK

    “Kama ukimkopesha mmojawapo wa watu wangu fedha ambaye ni mhitaji, usiwe kama mtu mkopesha fedha; usimtoze riba.

  17. Kutoka 22:26takriban 1491 KK

    Kama ukichukua vazi la jirani kama rehani, ulirudishe kwake kabla jua kuzama,

  18. Kutoka 22:27takriban 1491 KK

    kwa kuwa vazi lake ndilo pekee alilo nalo la kumfunika mwili wake. Ni nini kingine atajifunika nacho? Atakaponililia, nitasikia, kwa kuwa nina huruma.

  19. Kutoka 22:28takriban 1491 KK

    “Usimkufuru Mungu au kumlaani mtawala wa watu wako.

  20. Kutoka 22:29takriban 1491 KK

    “Usiache kutoa sadaka kutoka ghala lako au mapipa yako. “Lazima unipe mzaliwa wa kwanza wa wana wako.

  21. Kutoka 22:30takriban 1491 KK

    Ufanye vivyo hivyo kwa ngʼombe wako na kwa kondoo wako. Waache wakae na mama zao kwa siku saba, lakini siku ya nane unipe.

  22. Kutoka 22:31takriban 1491 KK

    “Ninyi mtakuwa watu wangu watakatifu. Kwa hiyo msile nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori; mtupieni mbwa.

  23. Kutoka 23:1takriban 1491 KK

    “Usieneze habari za uongo. Usimsaidie mtu mwovu kwa kuwa shahidi mwenye nia ya kudhuru wengine.

  24. Kutoka 23:2takriban 1491 KK

    “Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu,

  25. Kutoka 23:3takriban 1491 KK

    nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake.