Rukia maudhui

circa 1446 BC

Sinai & The Law

God meets Israel at Mount Sinai, reveals the Ten Commandments, and establishes the Tabernacle and the priestly covenant.

1,657 mistari · 2 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Kutoka 20:22takriban 1491 KK

    Kisha Bwana akamwambia Mose, “Waambie Waisraeli hivi: ‘Mmejionea wenyewe kwamba nimesema nanyi kutoka mbinguni:

  2. Kutoka 20:23takriban 1491 KK

    Msijifanyizie miungu yoyote na kuilinganisha nami, msijitengenezee miungu ya fedha wala miungu ya dhahabu.

  3. Kutoka 20:24takriban 1491 KK

    “ ‘Utanitengenezea madhabahu ya udongo, na juu yake utoe sadaka za kuteketezwa kwa moto na sadaka za amani, kondoo zako, mbuzi na ngʼombe zako. Popote nitakapofanya Jina langu liheshimiwe, nitakuja kwenu na kuwabariki.

  4. Kutoka 20:25takriban 1491 KK

    Ikiwa unanitengenezea madhabahu ya mawe, usiijenge kwa mawe ya kuchonga, maana mkitumia chombo cha kuchongea mtaitia unajisi.

  5. Kutoka 20:26takriban 1491 KK

    Msitumie ngazi kupandia kwenye madhabahu yangu, uchi wako usije ukadhihirika kwa chini.’

  6. Kutoka 21:1takriban 1491 KK

    “Hizi ndizo sheria utakazoweka mbele ya Waisraeli:

  7. Kutoka 21:2takriban 1491 KK

    “Kama ukimnunua mtumwa wa Kiebrania, atakutumikia kwa miaka sita. Lakini katika mwaka wa saba, atakuwa huru naye atakwenda zake pasipo kulipa chochote.

  8. Kutoka 21:3takriban 1491 KK

    Kama akija peke yake, atakwenda huru peke yake, lakini kama akija na mke, ataondoka pamoja naye.

  9. Kutoka 21:4takriban 1491 KK

    Kama bwana wake alimpatia mke naye akamzalia wana au binti, mwanamke pamoja na watoto wake watakuwa mali ya bwana wake na huyo mwanaume ataondoka peke yake.

  10. Kutoka 21:5takriban 1491 KK

    “Lakini kama mtumishi akisema, ‘Ninampenda bwana wangu, mke wangu pamoja na watoto na sitaki kuwa huru,’

  11. Kutoka 21:6takriban 1491 KK

    ndipo bwana wake atakapolazimika kumpeleka mbele ya waamuzi. Kisha atampeleka kwenye mlango au kizingiti na kutoboa sikio lake kwa shazia. Naye atamtumikia bwana wake maisha yake yote.

  12. Kutoka 21:7takriban 1491 KK

    “Kama mtu akimuuza binti yake kuwa mtumwa, hataachwa huru kama watumwa wa kiume waachiwavyo.

  13. Kutoka 21:8takriban 1491 KK

    Kama hakumpendeza bwana wake aliyemchagua, huyo bwana atamwacha akombolewe. Hatakuwa na haki ya kumuuza kwa wageni, kwa sababu huyo bwana atakuwa amekosa uaminifu.

  14. Kutoka 21:9takriban 1491 KK

    Kama akimchagua aolewe na mwanawe, ni lazima ampe haki za kuwa binti yake.

  15. Kutoka 21:10takriban 1491 KK

    Ikiwa huyo mwana aliyeozwa mtumwa mwanamke ataoa mwanamke mwingine, ni lazima aendelee kumtosheleza huyo mke wa kwanza kwa chakula, mavazi na haki zote za ndoa.

  16. Kutoka 21:11takriban 1491 KK

    Iwapo hatamtosheleza kwa mambo hayo matatu, huyo mke wa kwanza ataondoka na kuwa huru bila malipo yoyote ya fedha.

  17. Kutoka 21:12takriban 1491 KK

    “Yeyote ampigaye mtu na kumuua ni lazima auawe hakika.

  18. Kutoka 21:13takriban 1491 KK

    Hata hivyo, kama hakumuua kwa makusudi, lakini Mungu akaruhusu itendeke, basi atakimbilia mahali nitakapomchagulia.

  19. Kutoka 21:14takriban 1491 KK

    Lakini kama mtu akipanga na kumuua mwingine kwa makusudi, mwondoe katika madhabahu yangu na kumuua.

  20. Kutoka 21:15takriban 1491 KK

    “Yeyote amshambuliaye baba yake au mama yake ni lazima auawe.

  21. Kutoka 21:16takriban 1491 KK

    “Yeyote amtekaye nyara mwingine akamuuza au akamweka kwake, akikamatwa ni lazima auawe.

  22. Kutoka 21:17takriban 1491 KK

    “Yeyote atakayemlaani baba yake au mama yake ni lazima auawe.

  23. Kutoka 21:18takriban 1491 KK

    “Kama watu wakigombana na mmoja akimpiga mwingine kwa jiwe au kwa ngumi yake na hakufa bali akaugua na kulala kitandani,

  24. Kutoka 21:19takriban 1491 KK

    yule aliyempiga ngumi hatahesabiwa kuwa na hatia kama mwenzake ataamka na kujikongoja kwa fimbo yake, lakini hata hivyo, ni lazima amlipe fidia ya muda wake aliopoteza na awajibike mpaka apone kabisa.

  25. Kutoka 21:20takriban 1491 KK

    “Kama mtu akimpiga mtumwa wake wa kiume au wa kike kwa fimbo na mtumwa huyo akafa papo hapo, ni lazima aadhibiwe