Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. Warumi 7:15takriban 60 BK

    Sielewi nitendalo, kwa maana lile ninalotaka kulitenda, silitendi, lakini ninatenda lile ninalolichukia.

  2. Warumi 7:16takriban 60 BK

    Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, ni kwamba ninakubali kuwa sheria ni njema.

  3. Warumi 7:17takriban 60 BK

    Lakini, kwa kweli si mimi tena nitendaye lile nisilotaka bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

  4. Warumi 7:18takriban 60 BK

    Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lolote likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda.

  5. Warumi 7:19takriban 60 BK

    Sitendi lile jema nitakalo kutenda, bali lile baya nisilolitaka, ndilo nitendalo.

  6. Warumi 7:20takriban 60 BK

    Basi kama ninatenda lile nisilotaka kutenda, si mimi tena nifanyaye hivyo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.

  7. Warumi 7:21takriban 60 BK

    Hivyo naiona sheria ikitenda kazi. Ninapotaka kutenda jema, jambo baya liko papo hapo.

  8. Warumi 7:22takriban 60 BK

    Kwa maana katika utu wangu wa ndani naifurahia sheria ya Mungu.

  9. Warumi 7:23takriban 60 BK

    Lakini ninaona kuna sheria nyingine inayotenda kazi katika viungo vya mwili wangu inayopigana vita dhidi ya ile sheria ya akili yangu. Sheria hii inanifanya mateka wa ile sheria ya dhambi inayofanya kazi katika viungo vya mwili wangu.

  10. Warumi 7:24takriban 60 BK

    Ole wangu mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?

  11. Warumi 7:25takriban 60 BK

    Ashukuriwe Mungu kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu! Hivyo basi, mimi mwenyewe kwa akili zangu ni mtumwa wa sheria ya Mungu, lakini katika asili ya dhambi ni mtumwa wa sheria ya dhambi.

  12. Warumi 8:1takriban 60 BK

    Kwa hiyo, sasa hakuna hukumu ya adhabu kwa wale walio ndani ya Kristo Yesu, wale ambao hawaenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho.

  13. Warumi 8:2takriban 60 BK

    Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima katika Kristo Yesu imeniweka huru mbali na sheria ya dhambi na mauti.

  14. Warumi 8:3takriban 60 BK

    Kwa maana kile ambacho sheria haikuwa na uwezo wa kufanya, kwa vile ilivyokuwa dhaifu katika mwili, Mungu kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe kwa mfano wa mwanadamu mwenye mwili ulio wa dhambi na kwa ajili ya dhambi, yeye aliihukumu dhambi katika mwili,

  15. Warumi 8:4takriban 60 BK

    ili kwamba haki ipatikanayo kwa sheria itimizwe ndani yetu sisi, ambao hatuenendi kwa kuufuata mwili bali kwa kufuata Roho.

  16. Warumi 8:5takriban 60 BK

    Kwa maana wale wanaoishi kwa kuufuata mwili huziweka nia zao katika vitu vya mwili, lakini wale wanaoishi kwa kufuata Roho, huziweka nia zao katika mambo ya Roho.

  17. Warumi 8:6takriban 60 BK

    Kwa maana kuwa na nia ya mwili ni mauti, bali kuwa na nia inayoongozwa na Roho ni uzima na amani.

  18. Warumi 8:7takriban 60 BK

    Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui na Mungu, kwa maana haiitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.

  19. Warumi 8:8takriban 60 BK

    Wale wanaotawaliwa na mwili, hawawezi kumpendeza Mungu.

  20. Warumi 8:9takriban 60 BK

    Lakini ninyi, hamtawaliwi na mwili, bali na Roho, ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu. Mtu yeyote ambaye hana Roho wa Kristo, yeye si wa Kristo.

  21. Warumi 8:10takriban 60 BK

    Lakini kama Kristo anakaa ndani yenu, miili yenu imekufa kwa sababu ya dhambi, lakini roho zenu zi hai kwa sababu ya haki.

  22. Warumi 8:11takriban 60 BK

    Nanyi ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa, kwa njia ya Roho wake akaaye ndani yenu.

  23. Warumi 8:12takriban 60 BK

    Kwa hiyo ndugu zangu, sisi tu wadeni, si wa mwili, ili tuishi kwa kuufuata mwili,

  24. Warumi 8:13takriban 60 BK

    kwa maana mkiishi kwa kuufuata mwili, mtakufa, lakini kama mkiyaua matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.

  25. Warumi 8:14takriban 60 BK

    Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio watoto wa Mungu.