circa AD 48–96
Letters to the Churches
Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.
Mistari ya kipindi hiki
- 1 Wathesalonike 4:3takriban 54 BK
Mapenzi ya Mungu ni kwamba ninyi mtakaswe, ili kwamba mjiepushe na zinaa,
- 1 Wathesalonike 4:4takriban 54 BK
ili kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima,
- 1 Wathesalonike 4:5takriban 54 BK
si kwa tamaa mbaya kama watu wa Mataifa wasiomjua Mungu.
- 1 Wathesalonike 4:6takriban 54 BK
Katika jambo hili mtu asimkosee ndugu yake wala kumlaghai. Kwa kuwa Bwana ni mlipiza kisasi katika mambo haya yote, kama vile tulivyokwisha kuwaambia mapema na kuwaonya vikali.
- 1 Wathesalonike 4:7takriban 54 BK
Kwa maana Mungu hakutuitia uchafu, bali utakatifu.
- 1 Wathesalonike 4:8takriban 54 BK
Kwa hiyo, mtu yeyote anayekataa mafundisho haya hamkatai mwanadamu, bali anamkataa Mungu anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
- 1 Wathesalonike 4:9takriban 54 BK
Sasa kuhusu upendo wa ndugu hamna haja mtu yeyote kuwaandikia, kwa maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.
- 1 Wathesalonike 4:10takriban 54 BK
Nanyi kwa kweli mnawapenda ndugu wote katika Makedonia nzima. Lakini ndugu, tunawasihi mzidi sana kuwapenda.
- 1 Wathesalonike 4:11takriban 54 BK
Jitahidini kuishi maisha ya utulivu, kila mtu akijishughulisha na mambo yake mwenyewe na kufanya kazi kwa mikono yake, kama vile tulivyowaagiza,
- 1 Wathesalonike 4:12takriban 54 BK
ili maisha yenu ya kila siku yajipatie heshima kutoka kwa watu walio nje, ili msimtegemee mtu yeyote.
- 1 Wathesalonike 4:13takriban 54 BK
Lakini ndugu, hatutaki mkose kujua kuhusu wale waliolala mauti, ili msihuzunike kama watu wengine wasiokuwa na tumaini.
- 1 Wathesalonike 4:14takriban 54 BK
Kwa kuwa tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, na kwa hivyo, Mungu kwa njia ya Yesu atawafufua pamoja naye wale waliolala mautini ndani yake.
- 1 Wathesalonike 4:15takriban 54 BK
Kulingana na neno la Bwana mwenyewe, tunawaambia kwamba sisi ambao bado tuko hai, tuliobaki hadi kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia waliolala mauti.
- 1 Wathesalonike 4:16takriban 54 BK
Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Nao waliokufa wakiwa katika Kristo watafufuka kwanza.
- 1 Wathesalonike 4:17takriban 54 BK
Baada ya hilo sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili kumlaki Bwana hewani, hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
- 1 Wathesalonike 4:18takriban 54 BK
Kwa hiyo farijianeni kwa maneno haya.
- 1 Wathesalonike 5:1takriban 54 BK
Basi, ndugu, kwa habari ya nyakati na majira hatuna haja ya kuwaandikia,
- 1 Wathesalonike 5:2takriban 54 BK
kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajapo usiku.
- 1 Wathesalonike 5:3takriban 54 BK
Wakati watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka.
- 1 Wathesalonike 5:4takriban 54 BK
Bali ninyi, ndugu, hampo gizani hata siku ile iwakute ghafula kama mwizi.
- 1 Wathesalonike 5:5takriban 54 BK
Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku.
- 1 Wathesalonike 5:6takriban 54 BK
Kwa hiyo basi, tusilale kama watu wengine walalavyo, bali tukeshe na kuwa na kiasi.
- 1 Wathesalonike 5:7takriban 54 BK
Kwa kuwa wote walalao hulala usiku na wale walewao hulewa usiku.
- 1 Wathesalonike 5:8takriban 54 BK
Lakini kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukijivika imani na upendo kama dirii kifuani na tumaini letu la wokovu kama chapeo.
- 1 Wathesalonike 5:9takriban 54 BK
Kwa maana Mungu hakutuita ili tupate ghadhabu bali tupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.