Rukia maudhui

circa AD 48–96

Letters to the Churches

Paul and other apostles write to strengthen, correct, and encourage the scattered churches across the Roman world.

2,767 mistari · 21 vitabu vimehusishwa

Mistari ya kipindi hiki

Chuja kwa kitabu
  1. 1 Wathesalonike 5:10takriban 54 BK

    Yeye alikufa kwa ajili yetu ili hata kama tuko macho au tumelala, tupate kuishi pamoja naye.

  2. 1 Wathesalonike 5:11takriban 54 BK

    Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa.

  3. 1 Wathesalonike 5:12takriban 54 BK

    Sasa tunawaomba, ndugu, waheshimuni wale wanaofanya kazi kwa bidii miongoni mwenu, wale ambao wana mamlaka juu yenu katika Bwana na ambao wanawaonya.

  4. 1 Wathesalonike 5:13takriban 54 BK

    Waheshimuni sana katika upendo kwa ajili ya kazi zao. Ishini kwa amani ninyi kwa ninyi.

  5. 1 Wathesalonike 5:14takriban 54 BK

    Nasi twawasihi, ndugu, waonyeni walio wavivu, watieni moyo waoga, wasaidieni wanyonge na kuwavumilia watu wote.

  6. 1 Wathesalonike 5:15takriban 54 BK

    Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.

  7. 1 Wathesalonike 5:16takriban 54 BK

    Furahini siku zote;

  8. 1 Wathesalonike 5:17takriban 54 BK

    ombeni bila kukoma;

  9. 1 Wathesalonike 5:18takriban 54 BK

    shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu.

  10. 1 Wathesalonike 5:19takriban 54 BK

    Msiuzime moto wa Roho Mtakatifu;

  11. 1 Wathesalonike 5:20takriban 54 BK

    msiyadharau maneno ya unabii.

  12. 1 Wathesalonike 5:21takriban 54 BK

    Jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema.

  13. 1 Wathesalonike 5:22takriban 54 BK

    Jiepusheni na uovu wa kila namna.

  14. 1 Wathesalonike 5:23takriban 54 BK

    Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, awatakase ninyi kabisa. Nanyi mhifadhiwe roho zenu, nafsi zenu na miili yenu, bila kuwa na lawama katika Bwana wetu Yesu Kristo.

  15. 1 Wathesalonike 5:24takriban 54 BK

    Yeye aliyewaita ni mwaminifu naye atafanya hayo.

  16. 1 Wathesalonike 5:25takriban 54 BK

    Ndugu, tuombeeni.

  17. 1 Wathesalonike 5:26takriban 54 BK

    Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu.

  18. 1 Wathesalonike 5:27takriban 54 BK

    Nawaagizeni mbele za Bwana mhakikishe kuwa ndugu wote wanasomewa barua hii.

  19. 1 Wathesalonike 5:28takriban 54 BK

    Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi. Amen.

  20. 2 Wathesalonike 1:1takriban 54 BK

    Paulo, Silvano na Timotheo: Kwa kanisa la Wathesalonike mlio katika Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo:

  21. 2 Wathesalonike 1:2takriban 54 BK

    Neema na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo iwe nanyi.

  22. 2 Wathesalonike 1:3takriban 54 BK

    Ndugu, imetubidi kumshukuru Mungu kwa ajili yenu siku zote, kama ulivyo wajibu wetu, kwa sababu imani yenu inakua zaidi na zaidi na upendo wa kila mmoja wenu alio nao kwa mwenzake unazidi kuongezeka.

  23. 2 Wathesalonike 1:4takriban 54 BK

    Ndiyo sababu miongoni mwa makanisa ya Mungu, tunajivuna kuhusu saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote na dhiki mnazostahimili.

  24. 2 Wathesalonike 1:5takriban 54 BK

    Haya yote ni uthibitisho kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na kwa sababu hiyo ninyi mtahesabiwa kwamba mnastahili kuwa wa Ufalme wa Mungu, mnaoteswa kwa ajili wake.

  25. 2 Wathesalonike 1:6takriban 54 BK

    Mungu ni mwenye haki: yeye atawalipa mateso wale wawatesao ninyi