- English
- King James KJV
- Complete Jewish CJB
- World English WEBM
- Berean Standard BSB
- American Standard ASV
- Geneva GNV
- Young's Literal YLT
- Douay-Rheims DRC
- International
- Shqip ALB
- العربية SVD
- বাংলা BN-IRV
- မြန်မာ Judson
- 简体文 CUV-S
- 繁體中文 CUV-T
- Čeština BKR
- Nederlands STVE
- Français LSG
- Deutsch SCH
- Ελληνικά Vamvas
- ગુજરાતી GU-IRV
- Hausa HCB
- עברית Hebrew
- हिन्दी HCV
- Magyar KAROLI
- Bahasa Indonesia INDO-TB
- Italiano Diodati
- 日本語 Kougo
- 한국어 Korean
- മലയാളം MAL
- मराठी MRCV
- Norsk DNB
- فارسی OPV
- Polski BG
- Português Almeida
- Română Cornilescu
- Русский Synodal
- Español RVG
- Kiswahili Neno
- Svenska SV1917
- Tagalog TAG-ADB
- தமிழ் TCV
- తెలుగు TSA
- ภาษาไทย THAI-KJV
- Українська Ohienko
- Tiếng Việt CADMAN
- Yorùbá YCB
circa 1900–1700 BC
Jacob, Joseph & Egypt
Jacob wrestles with God and becomes Israel; Joseph is sold into slavery yet rises to save the world from famine.
Mistari ya kipindi hiki
- Mwanzo 49:20takriban 1689 KK
“Chakula cha Asheri kitakuwa kinono, naye atatoa chakula kitamu kimfaacho mfalme.
- Mwanzo 49:21takriban 1689 KK
“Naftali ni kulungu jike aliyeachiwa huru azaaye watoto wazuri.
- Mwanzo 49:22takriban 1689 KK
“Yosefu ni mzabibu uzaao, mzabibu uzaao ulio kando ya chemchemi, ambao matawi yake hutanda ukutani.
- Mwanzo 49:23takriban 1689 KK
Kwa uchungu wapiga mshale walimshambulia, wakampiga mshale kwa ukatili.
- Mwanzo 49:24takriban 1689 KK
Lakini upinde wake ulibaki imara, mikono yake ikatiwa nguvu, na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo, kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli,
- Mwanzo 49:25takriban 1689 KK
kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi, yeye anayekubariki kwa baraka za mbinguni juu, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi.
- Mwanzo 49:26takriban 1689 KK
Baraka za baba yako ni kubwa kuliko baraka za milima ya kale, nyingi kuliko vilima vya kale. Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu, juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake.
- Mwanzo 49:27takriban 1689 KK
“Benyamini ni mbwa mwitu mlafi mwenye njaa kuu; asubuhi hurarua mawindo yake, jioni hugawa nyara.”
- Mwanzo 49:28takriban 1689 KK
Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka inayomfaa.
- Mwanzo 49:29takriban 1689 KK
Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti,
- Mwanzo 49:30takriban 1689 KK
pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Abrahamu alinunua kwa ajili ya mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba.
- Mwanzo 49:31takriban 1689 KK
Huko ndiko Abrahamu na Sara mkewe walikozikwa, huko akazikwa Isaki na Rebeka mkewe, na huko nilimzika Lea.
- Mwanzo 49:32takriban 1689 KK
Shamba hilo na pango lililoko ndani yake lilinunuliwa kutoka kwa Wahiti.”
- Mwanzo 49:33takriban 1689 KK
Baada ya Yakobo kumaliza kutoa maelekezo hayo kwa wanawe, akarudisha miguu yake kitandani, akapumua pumzi ya mwisho, na akakusanywa kwa watu wake.
- Mwanzo 50:1takriban 1689 KK
Basi Yosefu akamwangukia baba yake, akalilia juu yake na akambusu.
- Mwanzo 50:2takriban 1689 KK
Ndipo Yosefu akawaagiza matabibu waliokuwa wakimhudumia, wamtie baba yake Israeli dawa ili asioze. Hivyo matabibu wakamtia dawa asioze,
- Mwanzo 50:3takriban 1689 KK
wakatumia siku arobaini, kwa maana ndio muda uliotakiwa wa kutia dawa ili asioze. Nao Wamisri wakamwombolezea Yakobo kwa siku sabini.
- Mwanzo 50:4takriban 1689 KK
Siku za kumwombolezea zilipokwisha, Yosefu akawaambia washauri wa Farao, “Kama nimepata kibali machoni penu semeni na Farao kwa ajili yangu. Mwambieni,
- Mwanzo 50:5takriban 1689 KK
‘Baba yangu aliniapisha na kuniambia, “Mimi niko karibu kufa; unizike katika kaburi lile nililochimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani.” Sasa nakuomba uniruhusu niende kumzika baba yangu, nami nitarudi.’ ”
- Mwanzo 50:6takriban 1689 KK
Farao akasema, “Panda, uende kumzika baba yako, kama alivyokuapiza kufanya.”
- Mwanzo 50:7takriban 1689 KK
Hivyo Yosefu akapanda kwenda kumzika baba yake. Maafisa wote wa Farao wakaenda pamoja naye, watu mashuhuri wa baraza lake na watu mashuhuri wote wa Misri.
- Mwanzo 50:8takriban 1689 KK
Hawa ni mbali na watu wote wa nyumbani kwa Yosefu, na ndugu zake, na wale wote wa nyumbani mwa baba yake. Ni watoto wao, makundi yao ya kondoo, mbuzi na ngʼombe tu waliobakia katika nchi ya Gosheni.
- Mwanzo 50:9takriban 1689 KK
Magari makubwa na wapanda farasi pia walipanda pamoja naye. Likawa kundi kubwa sana.
- Mwanzo 50:10takriban 1689 KK
Walipofika kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Atadi, karibu na Yordani, wakalia kwa sauti na kwa uchungu; Yosefu akapumzika huko kwa siku saba kumwombolezea baba yake.
- Mwanzo 50:11takriban 1689 KK
Wakanaani walioishi huko walipoona maombolezo yaliyofanyika katika sakafu ile ya kupuria ya Atadi, wakasema, “Wamisri wanafanya maombolezo makubwa.” Kwa hiyo mahali pale karibu na Yordani pakaitwa Abel-Mizraimu.