Skip to content

Mistari ya Biblia kuhusu Vows

136 mistari · 38 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, Hana akamchukua huyo mtoto, akiwa mdogo hivyo hivyo, pamoja na fahali wa miaka mitatu, efa ya unga na kiriba cha divai, naye akamleta mtoto kwenye nyumba ya Bwana huko Shilo.

  2. Utamwomba yeye, naye atakusikia, nawe utazitimiza nadhiri zako.

  3. Kwako wewe hutoka kiini cha sifa zangu katika kusanyiko kubwa, nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wakuchao wewe.

  4. Toa sadaka za shukrani kwa Mungu, timiza nadhiri zako kwake Yeye Aliye Juu Sana,

  5. na uniite siku ya taabu; nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”

  6. Ee Mungu, nina nadhiri kwako, nitakutolea wewe sadaka zangu za shukrani.

  7. Ee Mungu, kwa kuwa umesikia nadhiri zangu, umenipa urithi wa wale wanaoliogopa jina lako.

  8. Ndipo daima nitaliimbia sifa jina lako na kuzitimiza nadhiri zangu siku baada ya siku.

  9. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo. Ee Mungu, sifa zakungojea katika Sayuni; kwako wewe nadhiri zetu zitatimizwa.

  10. Nitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwa na kukutimizia nadhiri zangu:

  11. nadhiri ambazo midomo yangu iliahidi na nilizotamka kwa kinywa changu nilipokuwa katika shida.

  12. Wekeni nadhiri kwa Bwana Mungu wenu na kuzitimiza; nchi zote za jirani na walete zawadi kwa Yule astahiliye kuogopwa.

  13. Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote.

  14. Kifo cha watakatifu kina thamani machoni pa Bwana.

  15. Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako, mimi ni mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako; umeniweka huru toka katika minyororo yangu.

  16. Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru na kuliita jina la Bwana.

  17. Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana mbele za watu wake wote,

  18. katika nyua za nyumba ya Bwana, katikati yako, ee Yerusalemu. Msifuni Bwana.

  19. Aliapa kiapo kwa Bwana na akaweka nadhiri kwa Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo:

  20. “Sitaingia nyumbani mwangu au kwenda kitandani mwangu:

  21. sitaruhusu usingizi katika macho yangu, wala kope zangu kusinzia,

  22. mpaka nitakapompatia Bwana mahali, makao kwa ajili ya Yule Mwenye Nguvu wa Yakobo.”

  23. Ni mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake.

  24. Misemo ya Mfalme Lemueli, usia wa mama yake aliyomfundisha:

  25. “Ee mwanangu, ee mwana wa tumbo langu, ee mwana wa nadhiri zangu,