Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Sea

95 mistari · 55 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. nilipoamuru mipaka yake, na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake,

  2. niliposema, ‘Unaweza kufika mpaka hapa wala si zaidi; hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?

  3. Huvisukasuka vilindi kama sufuria kubwa ichemkayo, na kukoroga bahari kama chungu cha marhamu.

  4. Anapopita nyuma yake huacha mkondo unaometameta; mtu angedhani vilindi vilikuwa na mvi.

  5. maana aliiwekea misingi yake baharini na kuifanya imara juu ya maji.

  6. uliyenyamazisha dhoruba za bahari, ngurumo za mawimbi yake, na ghasia za mataifa.

  7. Bwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani; nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari,

  8. Mbingu na dunia zimsifu, bahari na vyote viendavyo ndani yake,

  9. Njia yako ilipita baharini, mapito yako kwenye maji makuu, ingawa nyayo zako hazikuonekana.

  10. Aliwanyeshea nyama kama mavumbi, ndege warukao kama mchanga wa pwani.

  11. Wewe unatawala bahari yenye msukosuko; wakati mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza.

  12. Bahari zimeinua, Ee Bwana, bahari zimeinua sauti zake; bahari zimeinua sauti za mawimbi yake.

  13. Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu, ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari: Bwana aishiye juu sana ni mkuu.

  14. Bahari ni yake, kwani ndiye aliifanya, na mikono yake iliumba nchi kavu.

  15. Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, imejaa viumbe visivyo na idadi, vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo.

  16. Huko meli huenda na kurudi, pia Lewiathani, uliyemuumba acheze ndani yake.

  17. Wengine walisafiri baharini kwa meli, walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu.

  18. Waliziona kazi za Bwana, matendo yake ya ajabu kilindini.

  19. Kwa maana alisema na kuamsha tufani iliyoinua mawimbi juu.

  20. Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini, katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka.

  21. Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono, mawimbi ya bahari yakatulia.

  22. Bwana hufanya lolote apendalo, mbinguni na duniani, katika bahari na vilindi vyake vyote.

  23. Mtukuzeni Bwana kutoka duniani, ninyi viumbe vikubwa vya baharini na vilindi vyote vya bahari,

  24. Nilikuwepo alipoziweka mbingu mahali pake, wakati alichora mstari wa upeo wa macho juu ya uso wa kilindi,

  25. wakati aliiwekea bahari mpaka wake ili maji yasivunje agizo lake, na wakati aliweka misingi ya dunia.