Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Providence of God

163 mistari · 41 vipengele

Mistari muhimu ya Biblia

Chuja kwa kitabu
  1. hakika, yeye alindaye Israeli hatasinzia wala hatalala usingizi.

  2. Wimbo wa kwenda juu. Wa Solomoni. Bwana asipoijenga nyumba, wajengao hufanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji, walinzi wakesha bure.

  3. Mnajisumbua bure kuamka mapema na kuchelewa kulala, mkitaabikia chakula: kwa maana yeye huwapa usingizi wapenzi wake.

  4. Ambaye humpa chakula kila kiumbe. Fadhili zake zadumu milele.

  5. Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, umenichunguza na kunijua.

  6. Unajua ninapoketi na ninapoinuka; unatambua mawazo yangu tokea mbali.

  7. Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; unaelewa njia zangu zote.

  8. Kabla neno halijafika katika ulimi wangu, wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana.

  9. Umenizunguka nyuma na mbele; umeweka mkono wako juu yangu.

  10. hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti.

  11. Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu, unikingaye kichwa changu siku ya vita:

  12. Bwana ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya.

  13. Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.

  14. Huwapa chakula mifugo na pia makinda ya kunguru yanapolia.

  15. katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyoosha mapito yako.

  16. Mkabidhi Bwana lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa.

  17. Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali Bwana huelekeza hatua zake.

  18. Kura hupigwa kwa siri, lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana.

  19. Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu, lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama.

  20. Hatua za mtu huongozwa na Bwana. Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe?

  21. Hakuna hekima, wala akili, wala mpango unaoweza kufaulu dhidi ya Bwana.

  22. Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita, bali ushindi huwa kwa Bwana.

  23. “Ole kwa Ashuru, fimbo ya hasira yangu, ambaye mkononi mwake ana rungu ya ghadhabu yangu!

  24. Ninamtuma dhidi ya taifa lisilomjua Mungu, ninamtuma dhidi ya taifa linalonikasirisha, kukamata mateka na kunyakua nyara, pia kuwakanyaga chini kama matope ya barabarani.

  25. Lakini hili silo analokusudia, hili silo alilo nalo akilini; kusudi lake ni kuangamiza, kuyakomesha mataifa mengi.