Rukia maudhui

Mistari ya Biblia kuhusu The Providence of God: Ruling the elements

9 mistari · 41 vipengele

Mistari kuhusu Ruling the elements

  1. Dhoruba hutoka katika chumba chake, baridi hutoka katika upepo uendao kasi.

  2. Pumzi ya Mungu hutoa barafu, eneo kubwa la maji huganda.

  3. Huyasheheneza mawingu kwa maji, naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo.

  4. Nayo mawingu huzungukazunguka pande zote kwa amri yake, juu ya uso wa dunia yote, kufanya lolote ayaamuruyo.

  5. Huleta mawingu ili kuadhibu wanadamu, au kuinyeshea dunia yake na kuonyesha upendo wake.

  6. Nilipokuja, kwa nini hakuwepo hata mmoja? Nilipoita, kwa nini hakuwepo hata mmoja wa kujibu? Je, mkono wangu ni mfupi mno hata nisiweze kuwakomboa? Je, mimi sina nguvu za kukuokoa? Kwa kukemea tu naikausha bahari, naigeuza mito ya maji kuwa jangwa; samaki wake wanaoza kwa kukosa maji na kufa kwa ajili ya kiu.

  7. Anakemea bahari na kuikausha, anafanya mito yote kukauka. Bashani na Karmeli zinanyauka na maua ya Lebanoni hukauka.

  8. Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu.

  9. Yohana alishuhudia habari zake, akapaza sauti, akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ ”